Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Mhando: Ikithibitika kuna ubadhirifu nitajiuzulu

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
MKURUGENZI Mkuu Shirika la Umeme nchini(Tanesco), Mhandisi William Mhando amesema kuwa ikigundulika kama kuna ubadhirifu wowote uliofanyika katika shirika hilo kutokana na Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali(CAG) basi atakuwa tayari kujiuzulu.


Mhando alisema hayo jana wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari katika mkutano wa kutoa ufafanuzi juu ya taarifa iliyotolewa na Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma(POAC) kwamba shirika hilo lilifanya ununuzi wa kati ya Sh300 bilioni hadi Sh600 bilioni kitu ambacho alidai si kweli na kimeleta matatizo.


Mhando alisema, shirika hilo limekuwa likipata hati safi baada ya ukaguzi na kwamba kama kuna chochote kitagundulika kuwa ni ubadhirifu basi atakuwa tayari kujiuzulu.


"Kama nimekosea niko tayari kujiuzulu na mwajiri akiamua kunihamisha sina tatizo na ninawaambia mimi sina miaka miwili kazini na shirika lina pata hati safi hilo muelewe na mliseme," alisema Mhando.


Kuhusu Jenereta ambalo liliagizwa litolewe nyumbani kwake alisema , mkataba wake wa kazi unaeleza kuwa anatakiwa kuwa na kifaa hicho hivyo alimwambia mwajiri wake hivyo na alimruhusu kuendelea kuwa nalo.
Akizungumzia ripoti ya POAC kuhusu matumizi ya fedha, Mhando alisema taarifa zilizotolewa kwa baadhi ya vyombo vya habari kuhusu Tanesco hazikuwa sahihi kwani kilichotolewa na kamati na kilichoandikwa kwenye vyombo vya habari si sahihi.


"Nimemwomba Mwenyekiti wa POAC, Zitto Kabwe atoe ufafanuzi kuhusu hilo kwa kuwa limetuletea matatizo kwenye sekta ya fedha ambayo tunaitegemea kufanya shughuli zetu," alisema Mhando.


Akizungumzia suala hilo, Zitto alisema kuhusiana na matumizi hayo ya Sh300 bilioni na Sh600 bilioni ambayo imesemekana yalifanyika ununuzi kinyume cha sheria imeleta matatizo kwani taarifa hizo zilizoenda kwenye umma hazikuwa sahihi.


"Hiyo imeleta shida kwenye taarifa ya kamati kwani hanzard za kamati taarifa haisemi hivyo na imewaletea shida Tanesco kwa kuwa wanahitaji mikopo kwenye taasisi za fedha," alisema Zitto.


Akitoa ufafanuzi alisema Tanesco walifanya ununuzi wa Sh258 bilioni na ni makubwa zaidi kuliko mashirika yote ya umma.


"Hawakufanya ununuzi kinyume cha sheria kwani kiasi hicho cha fedha tulichokitaja awali tulikuwa tunatoa mfano," alisema Zitto.

0 comments

Post a Comment