Msemaji wa baraza hilo la mawaziri Mohammed Hegazy amesema kwamba ombi lao la kujiuzulu bado halijakubaliwa na baraza la kijeshi linalotawala Misri.
Na wakati msemaji huyo alipokuwa akitoa taarifa,maelfu ya waandamanaji waliendelea kufika katika medani ya Tahrir.
Kufikia sasa zaidi ya watu 30 wameuwawa na wengine wapatao 1,800 kujeruhiwa kutokana na machafuko ya siku tatu yalioshuhudiwa katika mjini Cairo.
Wakereketwa na waandamanaji wamekuwa wakilishinikiza baraza kuu la kijeshi linalotawala kukabidhi mamlaka kwa serikali ya kiraia.
Lakini hatua ya baraza la mawaziri la kutaka kujiuzulu huenda ikaitumbukiza nchi hiyo katika mzozo zaidi wa kisiasa.
Tangazo la kutaka kujiuzulu litatafrisiwa kama ushindi kwa waandamanaji na huenda likawachochea kutoa matakwa zaidi .
Hii pia huenda ikalitatiza baraza kuu la kijeshi.Swali kubwa kwao ni Jee, walirudishe tena baraza hilo lililoomba kujiuzulu au wateuwe baraza jipya? lakini kwa vyovyote vile kutakuwa na shinikizo za kutaka serikali ya kiraia ipewe uwezo zaidi.
Katika kipindi kizima cha maandamano, baraza hilo la kijeshi limekuwa likilaumiwa kwa kujipa madaraka makubwa.
Jeshi lakubali kujizulu kwa baraza la mawaziri la Misri
Baraza la mawaziri nchini Misri limewasilisha hati ya kujiuzulu kuiongoza nchi hiyo kwa utawala wa kijeshi wakati ambapo kukiwa maandamano ya umma katika maeneo ya mji mkuu wa Cairo na kwengineko. Katika kauli yake aliyowasilisha kupitia televisheni ya taifa, msemaji wa serikali alisema serikali imekwishwa wasilisha taarifa ya kujiuzulu, lakini itaendelea na majukumu yake ya kila siku nchini humo katika kukabiliana na wakati mgumu. Hata hivyo kuna taarifa zenye utata juu ya mapakeo ya baraza la kijeshi la nchi hiyo kuhusu taarifa hiyo. Hatua hiyo inafuatia vurugu za siku tatu nchini humo kati ya vikosi vya usalama vya Misri na raia waandamanaji katika uwanja wa Tahrir. Zaidi ya watu 20 wameuwawa katika machafuko hayo. Mapema jana wanadiplomasia 140 wa Kiimisri waliyopo katika wizara za kigeni na balozi nje ya taifa hilo wametoa tamko lililotaka vikosi vya usalama viache kutumia nguvu dhidi ya raia wanaoandamana kwa amani.
0 comments