Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO , HABARI ZA MICHEZO - Fabregas ahamia Barcelona

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
ALIYEKUWA nahodha wa klabu ya Arsenal, Cesc Fabregas kwa sasa ni mchezaji rasmi wa Barcelona baada ya kusaini mkataba wa miaka mitano na mabingwa hao wa Ulaya.
Fabregas amefuzu uchunguzi wa afya yake aliofanyiwa mara mbili leo Jumatatu na atatambulishwa na klabu hiyo wakati wowote.

Uhamisho wa mchezaji huyo unakadiliwa kufikia paundi milioni 35, ambapo Arsenal itapokea kitita cha paundi milioni 30 na paundi milioni 5 nyingine zitatolewa kutegemea na idadi ya mechi atakazocheza na vikombe itakavyoshinda Barcelona.

Siku ya Jumapili, Arsenal na Barca walithibitisha makubaliano juu ya kumuuza mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 aliyedumu klabuni hapo kwa takribani miaka nane.

0 comments

Post a Comment