Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Wabunge Wasifu Uwezo Wa Kampuni ya IRIS Iliyoshinda Zabuni Ya Kutengeza Vitambulisho Vya Taifa

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Mheshimiwa Anna Abdalah,Kiongozi wa msafara wa Kamati Maalumu ya Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania,iliyopewa jukumu la kwenda nchini Malaysia,kuchunguza na kubaini uwezo wa Kampuni ya IRIS ya nchini humo,ili kubaini uwezo wa kampuni hiyo kutekeleza jukumu muhimu la kutengeneza vitambulisho vya Kitaifa. Mheshimiwa Anna Abdalla,alisema kuwa watanzania hawana sababu ya kuhofia uwezo wa kampuni hiyo kwani ni kampuni kubwa na ina wataamu na teknolojia ya hali ya juu ya kutengeza vitambulisho ambavyo ni vigumu mno kughushiwa na havichakai haraka.Alisema kuwa Kampuni ya IRIS imetengeza Vitambulisho vya Utaifa kwa nchi mbali mbali  Duniani.
Mbunge wa Maswa Mh. John Shibuda,akizungumza na waandishi wa habari jana mchana,Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam,mara baada ya kuwasili kutoka nchini Malaysia ambako  yeye na wabunge wenzake walikwenda kuchunguza sambamba na kubaini uwezo wa kampuni ya IRIS ya nchini humo iliyopewa zabuni ya kutengeza vitambulisho vya Kitaifa.Shibuda aliishauri serikali kutenga bajeti haraka kwa ajili ya kuanza mradi wa kutengeneza vitambulisho vya Kitaifa.Aliongeza kusema kuwa umuhimu wa  Watanzania kuwa na Vitambulisho vya Kitaifa haukwepeki.
Waheshiwa wabunge wakipata chai Jana asubuhi,mara baada ya kuwasili Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere,Dar es Salaam,wakitokea nchini Malaysia,ambako  walikwenda kuchunguza sambamba na kubaini uwezo wa kampuni IRIS,iliyoshinda na kupewa zabuni ya kutengeneza vitambulisho vya Kitaifa.
Baadhi ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakiwa katika picha ya pamoja. Picha  na Victor Makinda

0 comments

Post a Comment