IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Urusi na majeshi ya umoja wa nchi za kujihami za Ulaya Nato wanakutana kwa mazungumzo katika hoteli ya Sochi kusini mwa nchi hiyo, huku kipaumbele kikiwa ni mgogoro wa Libya.
Waziri wa mambo ya nje wa Urusi Sergei Lavrov alisema Urusi ilitaka kutumia baraza hilo kama "kichocheo cha ushirikiano".
Rais Dmitry Medvedev atakutana na mkuu wa Nato Anders Fogh Rasmussen.
Urusi imekuwa ikikosoa harakati za Nato nchini Libya, huku ikiyapa mazungumzo haya umuhimu wa kipekee.
Rais wa Afrika kusini Jacob Zuma naye atahudhuria, huku akiendelea kuongoza jitihada za upatanishi baina ya waasi na serikali mjini Tripoli baada ya waasi kukataa juhudi zilizofanywa na Umoja wa Afrika siku ya Jumapili.
Afrika kusini imekuwa mstari wa mbele katika jitihada za kufanya mazungumzo, na Rais Zuma anatarajiwa kukutana na Bw Medvedev, na huenda pia Bw Fogh Rasmussen, katika mkutano huo.
Matumizi ya makombora kama njia ya kujilinda nayo itajadiliwa kwenye mazungumzo hayo.
You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Urusi na Nato waijadili Libya
0 comments