Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Urusi na NATO, hazijaafikiana juu ya Libya

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Rais wa Urusi Dmitry Medvedev (kulia) na Katibu mkuu wa NATO Anders Fogh Rasmussen
Mkutano kati ya Urusi na Jumuia ya Kujihami ya NATO umemalizika kwa pande zote mbili kutoafikiana juu ya operesheni za kijeshi zinazofanywa nchini Libya.
Katika mkutano huo uliofanyika katika mji wa Sochi nchini Urusi, Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Urusi Sergei Lavrov ameituhumu NATO kwa kwenda mbele zaidi katika kulitafsiri azimio la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kuhusu Libya.
Urusi imeukosoa hasa uamuzi wa Ufaransa kuwapatia silaha waasi wa Libya.


Lakini hata hivyo Katibu mkuu wa jumuia hiyo ya NATO, Anders Fogh Rasmussen ametetea hatua hiyo kwa kusema kuwa itahitajika kwa ajili ya kuwalinda raia kutokana na mashambulio yanayofanywa na majeshi ya Libya yanayoongozwa na kiongozi wa nchi hiyo Muammar Gaddafi.


Aidha ametetea pia mpango wa jumuia hiyo wa kuunda mfumo wa kinga dhidi ya makombora barani Ulaya, ambao Urusi inaona ni kitisho kwa usalama wake.

0 comments

Post a Comment