Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - UBALOZI WA TANZANIA MOSCOW NCHINI URUSI WAWAAGA RASMI WAHITIMU RUSSIA

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

BALOZI WA TANZANIA NCHINI URUSI MH. JAKA MWAMBI AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI WALIOMALIZA MASOMO YAO NCHINI URUSI

UBALOZI WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA ULIOPO MOSCOW NCHINI URUSI UMEFANYA HAFLA FUPI YA KUWAAGA WANAFUNZI WALIOHITIMU MASOMO YAO NCHINI URUSI. KATIKA HOTUBA YAKE KWA WAHITIMU HAO, BALOZI WA TANZANIA NCHINI URUSI MH. JAKA MWAMBI AMEWAASA WAHITIU HAO KUZINGATIA TAALUMA WALIOIPATA KATIKA KUENDELEZA TAIFA LA TANZANIA. MH. MWAMBI AMESEMA SASA KUNA USHINDANI MKUBWA KWENYE SOKO LA AJIRA KUTOKANA NA UMOJA WA AFRIKA MASHARIKI. AMEWATAKA WAHITIMU HAO KUWA NGANGARI NA KUVUMILIA BAADA YA KURUDI NYUMBANI KWANI MWANZO NI MGUMU. KATIKA HOTUBA YAKE ILIYODUMU KWA MUDA WA DK. 48, MH. BALOZI ALISISITIZA KUTOPOTEZA MUDA MWINGI KATIKA KUCHAGUA KAZI BALI KURIDHIKA NA KILE AMBACHO KITAPATIKANA MARA TUU WATAKAPORUDI NYUMBANI TANZANIA. KATI YA WANAFUNZI WALIOHITIMU MASOMO YAO WAPO WALIOSOMEA TOURISM, HOSPITALITY AND SERVICE, MEDICINE, PHARMACY, ENGINEER NA ECONOMICS.

SEHEMU YA MAAKULI MARA BAADA YA HOTUBA YA MH. BALOZI
BAADA YA HAFLA HIYO FUPI ILIYOANZA MAJIRA YA SAA SABA MCHANA NA KUMALIZIKA SAA KUMI NA MOJA JIONI ILIKUWA NI HEPI BETHIDEI YA KUZALIA KWA MJUKUU WA BALOZI WA TANZANIA NCHINI URUSI MH. JAKA MWAMBI.
MTOTO DANIELA ALIYETIMIZA MWAKA MMOJA

MTOTO AKIWA ANATEMBEA
MAMA MZAZI WA MTOTO PROSCOVIA MWAMBI

0 comments

Post a Comment