Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO , HABARI ZA MICHEZO - Mashindano ya kula mjini Morogoro

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Wazo Ngosingosi ( kulia) akipokea zawadi kutoka kwa Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya ( watatu kulia) mara baada ya kuwa mtu wapili kumaliza shindano la kula chakula kilo moja ya wali,wakati wa maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, za kimkoa zilizofanyika Julai saba mwaka huu eno la Tarafa ya Lupiro, Wilaya ya Ulanga.
Washiriki wa Mashindano ya kula Wali kilo moja kwa muda wakipata maelezo kabla ya mashindano kuanza.
Maongezi ya hapa na pale.
Kipunga kikiwa tayari tayari kwa ajili ya washiriki wa mashindano.
kazi imeanza hapa.

Mchezo wa mashindano ya kula , ulibuniwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Issa Machibya, kwa ajili ya maadhimisho ya sherehe za miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara, ' Tanganyika' ambapo aliweza kununua mchele wa kutosha na kwa upende wa kitoweo cha nyama ya kuku , kuku walinunuliwa na Mkuu wa Wilaya ya Morogoro, Said Mwambungu.

Washiriki 14 walijitokeza kati ya hao wanawake walikuwa ni wanne , na ulifanyika siku ya kilele cha maadhimisho hayo ya kimkoa Julai saba, mwaka huu eneo la Tarafa ya Lupiro, Wilaya ya Ulanga na kuhudhiriwa na mamia ya wakati wa eneo hilo pamoja na viongozi wa serikali ngazi ya Wilaya na Mkoa .

Mshindi wa kwanza, Sudi Kilamilo alipatiwa sh: 35,000 na ngao , mshindi wa pili Wazo Ngosingosi , alizawadiwa sh: 25,000 na mshindi wa tatu , Omary Manjawa .Picha na John Nditi.

0 comments

Post a Comment