Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Uhalifu wa kutisha. Mwanafunzi achinjwa kama kuku

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
HOFU imetenda kwenye Shule ya Msingi Living stone ya mchepuo wa Kiingereza, wilayani Njombe, baada ya mwanafunzi Doris Lutego (12), aliyetekwa ndani ya bweni wiki iliyopita kukutwa ameuawa kwa kuchinjwa kama kuku, mwili wake kutenganishwa kichwa na kiwiliwili.
Mauaji ya mwanafunzi huyo yametokea siku chache baada ya polisi kutoa taarifa ya kutoweka kwa mwanafunzi huyo, kutokana na watu wasiojulikana kumteka ndani ya bweni.Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Evarist Mangalla, alisema mwili huo uliokotwa Juni 13, mwaka huu majira ya asubuhi, kichwa kilikutwa kimetupwa Mtaa wa Nzerengete, huku kikiwa kimewekwa kwenye mkoba wa daftari wa mwanafunzi huyo.
Mangala alisema kiwiliwili chake kilikutwa kimewekwa kwenye genge la biashara lililopo karibu na makazi ya Mwenyekiti wa Kitongoji cha Kambarage, kilomita 10 kutoka eneo la shule hiyo.
Awali, ilidaiwa mwanafunzi huyo alitekwa na watu wasiojulikana akiwa amelala baada ya kuvamia bweni la wasichana Juni 12, mwaka huu majira ya usiku na kutoweka naye, huku wakiacha jino na damu kwenye bweni.
Kutokana na uchunguzi wa polisi, watu watatu wanashikiliwa kwa tuhuma za kuhusika na mauaji hayo.
Alitaja wanaoshikiliwa kuwa, wote ni wakazi wa Njombe, mkoani Iringa.
Mangala alisema polisi inafanya uchunguzi wa kina kujua sababu za mauaji hayo ya kinyama, hasa yakishusisha mwanafunzi ambaye uchunguzi wa mwili wa marehemu unaonyesha kabla ya kuuawa, alipigwa na kitu kizito kichwani.
Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Sara Dumba, alisikitishwa na hali hiyo ambayo imesababisha hofu kwa wanafunzi wa shule hiyo na kwamba, wananchi wanapaswa kutulia wakati polisi wakiendelea na msako kubaini wahusika.
“Serikali imesikitishwa na mauji haya ya kinyama, ninachoomba wananchi wawe watulivu kwa wakati huu polisi wanafanya uchunguzi kubaini wahusika ili hatua za kisheria zichukuliwe,” alisema Dumba.
Baadhi ya wananchi walitaka serikali kuhakikisha usalama wa shule zote ambazo zimekuwa zikiweka bwenini wanafunzi, ili kuepusha matukio ya mauaji.
Augustino Wikesi, alisema kama shule hizo zingekuwa na ulinzi wa kutosha, mwanafunzi huyo asigetekwa usiku.

0 comments

Post a Comment