Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - Netanyahu akataa wito wa Obama kurejea kwenye mipaka ya 1967

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Rais wa Marekani Barack Obama na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu wamekutana mjini Washington kuujadili mchakato wa amani wa Mashariki ya Kati. Kufuatia mazungumzo hayo, Obama alikiri kuwa kulikuwepo tofauti za maoni kuhusu njia ya kupata amani katika kanda hiyo na akaongezea kuwa kwa Marekani, usalama wa Israel, ni suala la umuhimu mkubwa.
Mkutano wa viongozi huo umefanyika kufuatia mivutano iliyozuka baada ya Obama hivi karibuni kupendekeza kuwa taifa la Palestina litakaloundwa siku zijazo, liwe chini ya msingi wa mipaka iliyokuwepo kabla ya mwaka 1967. Netanyahu amepinga vikali pendekezo hilo. Amesema , anaamini kuwa Wapalestina watapaswa kukubali baadhi ya mambo yaliyokuwa hali halisi ya kimsingi. Israel ipo tayari kuafikiana ili kupata amani lakini haiwezi kurejea katika mipaka ya mwaka 1967, kwani mipaka hiyo haiwezi kulindwa. Vile vile mipaka hiyo haizingatii mabadiliko ya kijamii yaliyotokea katika kipindi cha miaka 44 iliyopita. Hata hivyo, Netanyahu amesema kuwa ataendelea kushirikiana na Obama kutafuta ufumbuzi wa amani utakaohakikisha usalama wa Israel.

0 comments

Post a Comment