Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KITAIFA , HABARI ZA LEO - Magufuli amteua Mfugale bosi Tanroads

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
WAZIRI wa Ujenzi, Dk John Magufuli, amemteua Patrick Mfugale kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara (Tanroads).


Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Balozi Harbert Mrango, uteuzi huo umefanyika kwa mujibu wa sheria ya wakala wa serikali ya mwaka 1997, kama ilivyorekebishwa mwaka 2009.


Kabla ya uteuzi huo, Mfugale alikuwa Kaimu Mtendaji Mkuu wa Tanroads na pia amewahi kushika nafasi mbalimbali katika serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Aliwahi kuwa Mhandishi mkuu mwenye majukumu maalumu katika Wizara ya Ujenzi na Mkurugenzi wa Idara ya Barabara za Mikoa.


Mhandisi huyo ana shahada ya uhandisi kutoka katika Chuo Kikuu cha Roorkee nchini India na shahada ya uzamili kutoka katika Chuo Kikuu cha Loughborough, Uingereza.


Taarifa hiyo ilisema mtendaji huyo mkuu, amewahi kusimamia ujezi wa barabara na madaraja muhimu hapa nchini.Uteuzi huo ni wa kipindi cha miaka mitatu na ulianza rasmi Mei 20 mwaka huu.

0 comments

Post a Comment