Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO - Ghasia za kidini zinazuka tena Misri

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Waziri Mkuu wa Misri, Essam Sharaf, amevunja safari ya kuzuru nchi za Ghuba baada ya ghasia kati ya Waislamu na Wakristo, zilizouwa watu kama sita.

Hii ilikuwa ziara muhimu kwa Waziri Mkuu, katika nchi za Ghuba ambazo zingeweza kutoa msaada anaohitaji sana, na nchi ambazo piya zina wasi wasi juu ya mwelekeo wa mapinduzi ya Misri.
Kwa kuvunja safari hiyo, Bwana Sharaf anaonesha anashughulishwa na ghasia nyengine zilizozuka baina ya makundi ya Waislamu na Wakristo.
Safari hii ghasia zimetokea kwenye mtaa wa kati-kati ya Cairo, pale kundi la Waislamu wa madhehebu ya Sunni, wanaoitwa Salafi, ambao hawapendi mabadiliko, lilipozingira kanisa ambamo likiamini Wakristo walikuwa wakimzuwia mwanamke, ambaye akitaka kubadilisha dini na kuwa Muislamu.
Risasi zilifyatuliwa, na kanisa na majengo mengine yalichomwa moto.
Ilichukua saa kadha kwa askari wa usalama kuzima mapigano.
Inafikiriwa kuwa Salafi ni wachache kati ya Waislamu, lakini wamekuwa na ghasia nyingi tangu Rais Hosni Mubarak kuondoka mwezi wa Februari.
Tangu wakati huo, kumetokea mapambano kadha baina ya Wakristo na Waislamu, na Wakristo wengi, ambao ni asili mia 10 ya watu wa Misri, wanahofia usalama wao, endapo makundi ya Waislamu wasiopenda mabadiliko, ndio yatashinda katika uchaguzi wa mwezi Septemba.

0 comments

Post a Comment