Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA KIMATAIFA , HABARI ZA LEO - EU kusherekea wiki yake kwa kujitolea

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

UMOJA wa Ulaya (EU), umezindua wiki ya umoja huo kwa kujishughulisha na shughuli mbalimbali za kujitolea nchini.Akizungumza jijini Dar es Salaam kwenye uzinduzi wa wiki hiyo jana, Mkuu wa umoja huo nchini, Balozi Tim Clarke, alisema katika wiki hiyo kutakuwa na shughuli mbalimbali zitakazofanyika nchini kwa ajili ya kukuza uelewa juu ya watu wanaojitolea.
Clark alisema shughuli hizo zitahusisha masuala yote, yakiwamo ya afya, elimu na mazingira, kaulimbiu ya mwaka huu itakuwa ni ‘Kujitolea’.“Huu ni wakati muafaka kwa Tanzania, wananchi wanaangalia mafanikio waliyoyapata katika kipindi cha miaka 50 ya uhuru, tunadhani ni vyema sisi pia tusherehekee juhudi za wale waliojitolea kwa ajili ya kuwasaidia  wengine,” alisema Balozi Clarke.

Balozi huyo alisema kila mtu anaweza kuleta mabadiliko na kutaka watu wajitolee muda wao, nguvu na ari na ujuzi wao wa maarifa kwa ajili ya kuwasaidia wengine ili kuleta mabadiliko.

Clark alisema shughuli zitakazofanywa katika wiki hiyo, ni kufanya usafi wa mazingira na kufukia mazalia ya mbu kwa ajili ya kujikinga na ugonjwa wa malaria, ambayo itafanyika katika masoko ya Kisutu na TX Kinondoni.Kwa mujibu wa balozi huyo, shughuli nyingine zitakazofanywa ni msafara wa baiskeli ambao utahusisha wanaume, wanawake, watoto, vijana, wazee na walemavu.
Alisema msafara huo wa baiskeli una lengo la kutoa elimu juu ya umuhimu wa kuboresha usalama barabarani kwa wapanda baiskeli.Pia, alisema shughuli hizo zitafanyika visiwani Zanzibar kwenye Shule ya Msingi Lumumba iliyoko Unguja, ambako kutatolewa mafunzo kuhusu usalama barabarani kwa wanafunzi, walimu na jamii inayozunguka shule hiyo.

0 comments

Post a Comment