Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO - Hakimu ajitoa kesi ya Manji,Mengi

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
HAKIMU Mkazi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es Salaam, Aloyce Katemana,  amejitoa katika kusikiliza kesi ya madai ya fidia ya Sh1, iliyofunguliwa na mfanyabiashara maarufu wa jijini, Yusuph Manji, dhidi ya Mwenyekiti wa IPP, Reginald Mengi.

Katemana alitangaza  uamuzi huo jana ambapo alisema amefanya hivyo kwa hiyari yake.Hatua hiyo ilikuja baada ya wakili wa Manji, Dk Ringo Tenga,  kuiambia mahakama kuwa  kesi ilifikishwa kwa ajili ya kutajwa.

Lakini kabla wakili huyo hajaendelea na maelezo,Hakimu Katemana alimkatisha na kutangaza uamuzi wa kujitoa kusikiliza kesi hiyo na hakutoa sababu za kufikia uamuzi huo.

Baada ya kutangaza kujitoa, Hakimu Katemana aliahirisha  kesi hiyo hadi Aprili 15 mwaka huu, itakapotajwa ten.
Pia siku itakuwa ya kujulikana kama imepangia hakimu mwingine au la.

Kujitoa kwa hakimu katika kesi hiyo, kumekuja siku kadhaa baada ya Mahakama Kuu, Kanda ya Dar es Salaam kurejesha jalada la kesi hiyo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kuamuru iendelee kusikilizwa na hakimu huyo.

Jalada hilo lilipelekwa katika Mahakama Kuu kufuatia hatua ya wakili wa Mengi, Michael Ngalo,kuandika barua akilalamikia namna kesi hiyo inavyoendeshwa na hakimu Katemana.Katika barua hiyo ya Februari 23 mwaka huu, Ngalo alidai kuwa Hakimu Katemana anaegemea upande mmoja na kwamba hata uamuzi wake wa Februari 11 mwaka huu, ulikuwa wa mashaka.

Hivyo alimuomba Jaji Mfawidhi, Semistocles Kaijage, alipitie jalada la kesi hiyo.Jaji Kaijage alilipitia jalada hilo na kuagiza lirudishwe Kisutu na kesi iendelee kusikilizwa na hakimu Katemana.Hatua hiyo ilikuja baada ya jaji kujiridhisha kuwa hakukuwa na ukiukwaji wa taratibu za kisheria.

Pamoa na kutoa agizo hilo, Jaji Kaijage pia aliushauri upande wa Mengi uombe hakimu ajionde kama utakuwa haiakuridhika na uamuzi wake.Kabla ya uamuzi  wa Februari 11 mwaka huu,   wakili wa Yusuph Manji, Mabere Marando, aliiomba Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, isipokee nyaraka zilizowasilishwa na Mengi kwa maelezo kuwa hazikuwa za msingi katika kesi hiyo.

Marando pia aliutaka upande wa Mengi ueleze mahali ulikopata  risiti za malipo za ya serikali, kuhusu Kampuni ya Quality Finance Cooparation Group na mtu aliyewapa.Katika ushahidi wake kwenye kesi hiyo, Manji, alitumia mkanda wa video badala ya kuzungumza.

Mkanda huo wa picha wa(DVD), ulionyesha hotuba ya Mengi wakati akizungumza na waandishi wa habari na kumtaja Manji kuwa miongoni mwa mafisadi papa, wanaoihujumu nchi.Mkanda huo ulionyeshwa katika mahakama ya wazi, iliyokuwa imeketi chini ya Hakimu Katemana.

Katika mkanda huo Mwenyekiti wa IPP, alisikika akiwataja watu watano wanaotuhumiwa kwa ufisadi mkubwa hapa nchini na kuitaka serikali iwashughulikie haraka, ili kuinusuru nchi isiyumbishwe.

Mengi aliwataja watu wengine aliowaita kuwa ni mafisadi papa kuwa ni pamoja na Mbunge wa Igunga na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CC-CCM) na Halmashauri Kuu ya Chama hicho (NEC-CCM) Taifa, Rostam Aziz. Hali kadhalika wafanyabiashara, Tanil Somaiya, Jeetu Patel na Subash Patel, ambao alisema wanatuhumiwa kuiba mabilioni ya wananchi na kuzihamishia nje ya nchi. 
mwisho

0 comments

Post a Comment