Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - HABARI ZA LEO - Uganda yamkaribisha Gadhafi

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Msemaji wa rais wa Uganda amesema kiongozi wa Libya, kanali Muammar Gaddafi anakaribishwa nchini Uganda. Kwa mualiko huo, Uganda inaonekana kuwa nchi ya kwanza kusema itamkaribisha Gaddafi. Msemaji wa rais Yoweri Museveni, Tamale Mirundi, ameliambia shirika la habari la Associated Press hii leo, kwamba sera ya Uganda ni kuwapa ukimbizi wanaowasilisha maombi yao kuishi uhamishoni nchini humo. Aidha Mirundi amesema sera hiyo ipo kwa sababu raia wengi wa Uganda waliikimbia nchi wakati wa utawala wa dikteta Iddi Amin. Televisheni ya al Arabiya iliripoti kwamba Uganda ingemkaribisha Gaddafi baada ya nchi za magharibi na mataifa mengine kupendekeza aende uhamishoni, lakini haikutoa taarifa zaidi. Naibu waziri wa mambo ya nchi za kigeni, Henry Okello Oryem, amekanusha ripoti hizo akisema ni uvumi. Hata hivyo amesema wameijadili Libya leo kwenye kikao cha mawaziri, na Uganda itamruhusu Gaddafi kuishi uhamishoni nchini humo iwapo atawasilisha ombi lake.

0 comments

Post a Comment