Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mrema aiibua wizi wa 914 Milion Rombo

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
KAMATI ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC), imeagiza kusimamishwa kazi mara moja kwa watumishi 12 wa Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, mkoani Kilimanjaro, wanaotuhumiwa kuhusika na upotevu wa Sh914 milioni.
 Kamati hiyo inayoongozwa na Mbunge wa Vunjo, Agustino Mrema, pia imeagiza watumishi hao wakamatwe na kufikishwa polisi kabla ya kumalizika kwa siku ya jana.

Hali kadhalika, imebariki uamuzi wa kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Wilaya ya Rombo, kilichofanyika  Februari 7 mwaka huu, kuwa yalikuwa halali.Kikao hicho kilikuwa  chini ya mwenyekiti wake,Anthony Tesha.Watumishi walioamriwa kukamatwa ni pamoja Mweka Hazina wa halmashauri hiyo, Emanuel Masele, Ofisa Elimu  (Taaluma), Godfrey Kabyemera. Mhandisi, Elias Mshana na Mhasibu Eric Barongo.

Wengine na nyadhifa zao zikiwa katika mabano ni, Felician Msangi(Mhandisi), Perer Muganda (Mhasibu),Silvia Shirima na Rachel Mshangila (Maofisa Ugavi Wasaidizi), Remid Asenga (Fundi Mchundo) na Abdallah Mruma(Mwalimu) Orodha hiyo pia inamjumuisha Ofisa Elimu ya Msingi, Joseph Ngoseki, ambaye alihamishiwa katika Mkoa wa Geita na Alfonce Kasanyi, ambaye kwa sasa anafanya kazi katika Halmashauri ya Wilaya ya Siha.

Hata hivyo, kamati  imeagiza maofisa hao wawili wakamatwe na kurejeshwa wilayani Rombo, kujibu tuhuma zinazowakabili.Pia imeshauri Katibu Mkuu katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa), kuchukua hatua dhidi ya maofisa hao.“Mkurugenzi tunakuagiza uwape barua zao za kusimamishwa kazi leo  (jana) na uhakikishe ikifika jioni umeshawakabidhi polisi. Wakae nje ya ofisi za umma wakati uchunguzi ukiendelea,”alisisitiza Mrema.

Uamuzi wa kamati hiyo ulikuja baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji  kuhusu taarifa ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali.Ukaguzi huo ni ule uliofanywa katika kipindi cha kati ya Juni na Julai mwaka 2009 na kufichua wizi na ubadhirifu wa Sh914 milioni.

Katika taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo,Samwel Kibaja aliwaambia wabunge kuwa ameshindwa kutekeleza agizo la Baraza la madiwani kuhusu kuwasimamisha kazi watumishi hao, kwa kuhofia athari za kisheria.Kauli hiyo ilionekana kuwachefua wajumbe wa kamati, ambao walisema uamuzi wa baraza, hauwezi kubatilishwa na mkurugenzi  na kwamba kama aliona kuwa kuna tatizo alipaswa alirudishe suala hilo barazani.

Wajumbe wengine wa kamati hiyo ni Godfrey Zambi ambaye ni Mbunge wa Mbozi Mashariki na wabunge wa viti maalum Subira Mgalu na Tauhida Cassian Galos walisema wizi uliofanyika Rombo ni wa wazi.Katika kikao hicho cha kamati, Mbunge Tauhida Casian Galos alitahadharisha kuwa maamuzi ya LAAC juu ya kusimamishwa kazi na kukamatwa kwa watuhumiwa hao yasipuuzwe.
Tags:

0 comments

Post a Comment