Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Msafara wa mama Kikwete wapataa ajali, dereva afariki

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
MOJA wa madereva waliokuwa kwenye msafara wa Mke wa Rais Jakaya Kikwete, Salma, amekufa papo hapo baada ya gari alilokuwa akiendesha kugongwa na gari jingine katika ajali iliyohusisha magari matatu mkoani Pwani.

Ajali hiyo imetokea jana majira ya saa 6:00 mchana eneo la Ruvu Darajani, wakati msafara wa mama Salma ukitokea Dar es Salaam kwenda Chalinze, wilayani Bagamoyo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani, Absalom Mwakyoma, alithibitisha tukio hilo na kwamba, ajali hiyo ilihusisha magari matatu likiwamo la Ikulu.

Mwakyoma alisema jina la dereva aliyekufa litatajwa baadaye, huku akieleza kuwa ajali hiyo ilitokea baada basi kugonga kwa nyuma Hiace, kisha lilihamia upande wa kulia na kubamiza gari ya Ikulu iliyokuwa ikisindikiza msafara.

Alisema watu wengine walinusurika na kwamba, uchunguzi zaidi unaendelea kuhusiana na tukio hilo.
Tags:

0 comments

Post a Comment