ASKARI WAFUTA PICHA KWENYE KAMERA ZA WAANDISHI WA MWANANCHI
KAMA kweli mabomu hayana macho, wala hayaogopi cheo cha mtu. Hilo limedhirika baada ya makombora mawili yaliyoruka hewani naada ya milipuko kutokea katika maghala ya silaha ya kambi ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), Gongo la Mboto, jijini Dar es Salaam kutua nyumbani kwa Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, eneo la Pugu.
Hata hivyo, milipuko hiyo ilipotokea usiku Jumatano iliyopita na kuua watu zaidi ya 40 na kuwacha wengine majeruhi zaidi ya 300, Pinda alikuwa kwenye bungeni mjini Dodoma.
Siku ya Alhamisi, Mwananchi Jumapili lilishuhudia mabaki ya kombora moja yaliyosababisha kiwewe kwa waliokuwawemo ndani ya nyumba hiyo iliyopo Kimani, Pugu karibu na machimbo ya mchanga lakini waandishi walipoenda juzi walikuta askari wa JWTZ wameyachukua na kuacha alama mahali yalipofiga.
Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Msaidizi wa Shughuli za nyumbani kwa Waziri Mkuu, Pascal Mnally alisema makombora hayo yalitua nyumbani hapo kati ya saa 3:00 usiku na saa 4:00 usiku.
Mnally alisema baada ya makombora hayo kuangukia hapo yalizua taharuki na kiwewe kwa familia ya Waziri Mkuu huyo.
"Baada ya kishindo cha mabomu, familia yake ilitoka nje na kuanza kukimbia bila mwelekeo maalumu, lakini yeye alibakia ndani kusubiri kitakachotokea,” alisema Mnally na kusisitiza:
"Mimi sikukimbia, majira ya usiku nilipigiwa simu na Mzee (Waziri Mkuu) akiniulizia hali yangu na familia yangu, nikamwambia tuko salama, isipokuwa mama (mke wangu) amekimbia na sijui wamekimbilia wapi.
"Mzee akaniambia, kuwa hatukupaswa kukimbia ovyo na alitutaka tusiondoke kwa sababu tukikimbia ovyo tunaweza kupata madhara makubwa”.
Akionyesha mahali yaliangukia, Mnally alisema: "Kwa kweli hali ilikuwa inatisha. Kwenye saa 3:00, 4:00 usiku hivi ndipo makombora yakaanguka hapa. Moja lipiga hapa (alionyesha na tawi la mwembe uliokatwa kwa kombora hilo) na lilikuwa kubwa kweli kweli.
"Lingine lililoangukia hapa (anaonyesha shimo) lakini lilikuwa dogo tofauti na na la pale”.
Kurudi familia
Baada ya hapo Mnally alimwonyesha mtoto wake aliyekimbi: "Huyu naye karudi jana asubuhi, alisema walikimbilia Vigama mbele ya Stesheni ya Reli ya Tazara."
Alifahamisha saa 10:00 alfajiri siku Alhamisi alikuwa peke yake nyumbani bila ya kujua familia yake ilala wapi, lakini baadaye waliokimbia walirudi nyumbani wakiwa salama.
Alisema askari wa Jeshi la Wananchi wa Tanzania walifika nyumbani juzi kuyaondoa makombora hayo, lakini wakawapa tahadhari kuwa wasiende maeneo ya msitu mdogo uliopo jirani na nyumba hiyo ambalo ni eneo la Waziri Mkuu pia kwa sababu ya usalama wao kwa vile kuna uwezekano kukawa na mabomu mengine kuangukia huko.
Askari wanyang’anya kamera
Katika hali isiyo ya kawaida, waandishi wa habari wa Mwananchi Jumapili ilifika kupiga picha katika nyumba hiyo, askari waliokuwepo eneo hilo walimnyang'nya kamera mpigapicha na kufuta picha zote zilizopigwa zikiwemo za matukio mengine.
Askari hao kuwaamru waandhi hao kuondoka mara moja katika eneo hilo kwa kuwa hakuwa na mwaliko wa kuingia katika nyumba hiyo ya Waziri Mkuu.
Wananchi milimani
Siku ya tukio wakazi wa maeneo hayo ikiwamo Pugu Kigogo Fresh, Kwa Chanza na Pugu Stesheni ya Tazara walikimbilia milimani ikiwemo katika eneo hilo la Waziri Mkuu huku wengine wakijibanza kwenye mahandaki ya mashimo ya kokoto na mchanga yaliyopo Golani.
Usiku huo, Mwananchi Jumapili iliyokuwa eneo la tukio, ilishuhudia makombora zaidi ya 20 yakitua kwenye msitu uliopo karibu na nyumbani kwa Pinda.
Hata hivyo, wakati wananchi wanaanza kurejea nyumbani kwao saa 6:48 usiku siku hiyo, Mwananchi Jumapili iliona gari moja aina ya Toyota Land Cruiser lililokuwa na usajili wa namba za STK likiwa mwendo kasi kuelekea nyumbani kwa Waziri Mkuu likiwa lina watu kadhaa.
Wakati uharibifu na vifo vikitokea maeneo ya Gongolamboto, kombora moja lilitua nyumbani kwa Athumani Chabwalika maeneo ya Pugu kwa Chanzi na kusababisha nyumba yote kuteketea kwa moto.
Makombora mengine aliangukia Kitunda, machimbo, Kisarawe, Mbagala, Kigamboni, Tabata Segerea, Kimanga, Pugu Kichangani, Mwisho wa Lami na Pugu Kwalala, Majohe na Kipunguni.
Kwa mujibu wa JWTZ, jumla ya magahala ya silaha 23 yaliteketea kwa moto na kwamba sasa wanafanya kazi ya kukusanya mabaki ya mabomu yaliopo katika makazi ya watu.

![](http://www.blogger.com/img/icon18_edit_allbkg.gif)
0 comments