Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kilichotokea Kwenye Maandamano Arusha:

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Tafsiri kwa hisani  Ya Global Publishers


Mchumba wa DK Slaa, Bi Josephine Mshumbusi akivuja damu baada ya kujeruhiwa jana
Ndugu Zangu,
JUMA lililopita Watanzania, na dunia pia, tuliona kupitia televisheni na vyombo vingine vya habari, picha zikiwaonyesha polisi wetu wakipambana na waandamanaji wafuasi wa Chama Cha Wananchi, CUF. Ilisikitisha sana.

Pengine polisi ‘kupambana’ na waandamanaji si neno sahihi. Mara nyingi tunachokiona ni polisi ’kuwaandama’ waandamanaji. Hii ni pamoja na polisi kuwatawanya waandamanaji kwa virungu, mabomu ya machozi, risasi za mipira na hata za moto.

Jana tena, Watanzania na dunia, tumeona picha za televisheni zikiwaonyesha polisi wetu wakipambana ama kuwaandama waandamanaji wafuasi wa CHADEMA kule Arusha . Imeripotiwa na BBC kuwa kuna Watanzania waliopoteza maisha. Inasikitisha sana. Na unapoangalia picha hizi zenye kuharibu taswira njema ya nchi yetu ndani na nje ya mipaka yetu unajiuliza; KWANINI?
Mwenyekiti na Mbunge wa Hai, Freeman Mboe akiwa chini ya ulinzi

Kinachonijia haraka kichwani ni hofu ya mfumo. Linanijia pia neno ´MAANDAMANO´. Afrika MAANDAMANO ni neno baya sana ukilitamka mbele ya watawala. Kuandamana ni 'kuiandama' Serikali. Ni kama ilivyokuwa katika nchi za Kikomunisti kabla ya kuangushwa kwa ukuta wa Berlin. Kwa wasiojiamini ndani ya mifumo ya kiutawala Afrika, kuandamana ni sawa na kutaka ´Kuuvunja Ukuta´. Na kwa watu wa nchi zetu hizi, nao wameanza kuuona ukuta.

Kwa watawala Afrika, hakuna msamiati wa ’ Maandamano’ , kuna ’ MATEMBEZI ya MSHIKAMANO’. Afrika hakuna dhambi ya kuandamana kuunga mkono au kupongeza kauli au jambo lililotendwa na upande wa utawala. Dhambi ni kuandamana kupinga. Tujiulize tena; nini maana ya maandamano?

Tunaamini katika demokrasia, maandamano ni namna pia ya kujieleza. Muhimu katika maandamano ni kuhakikisha kuwa yanakuwa ni ya amani na utulivu. Wenye kuandamana waandamane na wengine waendelee na shughuli zao. Na hapa ni jukumu la wenye kuandaa maandamano kwa kuwashirikisha polisi.

Kuwepo na utaratibu unaoeleweka. Wapi waandamanaji watakusanyikia kabla ya kuanza maandamano. Hivyo basi, wapi maandamano yataanzia, umbali wa kilomita ngapi, kwa kupita barabara zipi na wapi yataishia. Hayo yanaweza kufanyika kwa ustaarabu kabisa.

Jukumu la polisi litakuwa ni kuyaongoza na kuhakikisha hakuna vurugu zinazotoka miongoni mwa waandamanaji, na si kinyume chake. Kwanini kuwepo na hofu ya vurugu wakati wenye kuandamana ni wafuasi wa chama au kikundi kimoja cha kijamii kwa wakati mmoja, tena wakiwa na viongozi wao?
Katika nchi za wenzetu, polisi huwa na kazi ngumu na hata kufikia kuwaambia waandaaji wa maandamano kusitisha maandamano kama maandamano husika yatasababisha kuwepo na maandamano ya kupinga maandamano hayo katika wakati mmoja kutoka kwa kundi lingine. Sisi hatujafikia huko. Kwa mfano, Dar wafuasi wa CUF wakiandamana kwa amani, wafuasi wa CCM huwaoni kufanya maandamano ya kuwapinga CUF kwa wakati huo huo, na kinyume chake.
Mchumba wa DK. Slaa, Bi. Josephine
Dunia imebadilika, tunahitaji kubadilika pia. Jeshi letu la polisi lijipange upya. Kwa jinsi picha za televisheni zinavyoonyesha polisi wetu wanavyowapiga virungu na hata kuwarushia risasi waandamanaji wasio na silaha inaamsha hisia mbaya kwa Watanzania. Inaleta taswira mbaya ya nchi yetu kwa jumuiya ya kimataifa. Inasikitisha sana. Ni aibu kwa nchi yetu tuliyozaliwa na tunayoipenda sana. Tubadilike.
Maggid,
Iringa
http://mjengwa.blogspot.com

PICHA: JOSEPH NGILISHO-ARUSHA/GPL
Comment

You need to be a member of Global Publishers to add comments!



GeorgeComment by George 6 hours ago
hakyanani hi ndo tanzania yetu yenye amani na upendo
Tariq JumanneComment by Tariq Jumanne 7 hours ago
Duh! hii kali!
UngujaukuuComment by Ungujaukuu 7 hours ago
Waziri mwenye shamana na IGP mnatakiwa mjiuzulu na muombe radhi umma wa Watanzania, IGP Mwema ulisema jeshi lako ni la kisasa, na nia ni kufanya raia wasione askari ni adui kwao, lkn leo hii polisi wanashambulia raia wasio na siraha kwa risasi za moto,mabomu ya machozi,virungu.
Athari zake nadhani mmeanza kuziona, watalii wanaondoka, Arusha si Geneva ya Afrika tena, hapakaliki. Hotel zitakosa wageni, ongezeko la wasio na ajira litaongezeka, na bila shaka idadi ya uhalifu itaongezeka, maana hakuna shughuli za kitalii tena mjini Arusha na kurudisha tena halii hii ndo mpaka Jk aende kuwaangukia wazungu hawa kwamba jamani njooni, Tanzania ina amani.,viongozi wetu acheni kufikiria kama funza...tunapoamua kufanya jambo tufikirie mara mbili kabla ya kutenda.
Zanija KanjundaComment by Zanija Kanjunda 7 hours ago
HUYU MAMA ANASTAHILI KUITWA MWANAMKE SHUJAA WA SIASA TANZANINIA! HAKI HAIPATIKANI MPAKA DAMU IMWAGIKE NA NDIO TUNACHOKIONA HAPA MUNGU WABARIKI WAPINZANI WA SAIASA ZA TANZANIA.
kokusimaComment by kokusima 8 hours ago
nivigumu kuamini Sebastian, wapi tunakwendaangalia video kwa michuzi. tuombe sana.
godwinComment by godwin 8 hours ago
fight chadema tupo nyuma yenuuuuuuuuu
SamComment by Sam 8 hours ago
Natamani sana hii makala angeisoma Makamba, Jk, Said Mwema, na wenzao...
Mvuruga amani hapa si mwingine bali yuleyule anayejinadi kuilinda hiyo amani-SERIKALI.
Kuna mantiki gani kuwashambulia kwa risasi za moto na mabomu watu wanaoandamana kwa amani, wasio na silaha yeyote, waliofunga vitambaa vyeupe mikononi kama ishara ya amani,na ambao sheria inawaruhusu kufanya maandamano wakati wowote wanaotaka, sharti likiwa moja tu kuwajulisha polisi saa 48 kabla ya wao kuandamana, sharti ambalo walilitekeleza?
HILI LA KUPIGA RAIA HAKIKA HALIKUBALIKI KATIKA NCHI YEYOTE YA WATU WENYE KUHESHIMU UHURU NA UTU WA WATU WAO
Sebastian Salatiel ShemhiluComment by Sebastian Salatiel Shemhilu 9 hours ago
HII NI TANZANIA KWELI?
Tags:

0 comments

Post a Comment