HATIMAYE kitendawili cha nani kuwa Meya wa Kigoma Ujiji kimetenguliwa rasmi baada ya mgombea wa chama cha Chadema Bakari Hussein kumuangusha mgombea wa CCM John Rutabiirwa katika uchaguzi uliofanyika jana.
Ushindi huo umekiwezesha chama hicho kikuu cha upinzani nchini kuongoza halmashauri tano had sasa, nyingine zikiwa ni Karatu, Ukerewe, Moshi Mjini na Musoma Mjini. Chaguzi katika miji ya Arusha na Mwanza bado zina utata.
Mjini Kigoma ulikuwa ni mvutano wa aina yake ambao uliodumu kwa kwa takribani wiki mbili kati ya vyama hivyo viwili na hatimaye umemalizika kwa amani baada ya kufahamika nani mshindi wa kiti hicho.
Bakari Hussein Beji wa Chadema alimshinda Mgombea wa CCM, John Rutabiirwa na hivyo kumaliza mivutano iliyosababisha kuahirishwa kwa uchaguzi wa mwanzo uliopangwa kufanyika Desemba 17 mwaka huu. Beji alipata kura 15 dhidi ya kura 12 alizopata mgombea wa CCM ambapo katika hali iliyowashangaza wengi, kura moja iliharibika kiasi cha kuzua minong'ono kwamba kuna hali ya kuhujumiana baina ya Wajumbe wa Baraza hilo la Madiwani.
Aidha katika nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa Manispaa hiyo, Yunus Ruhomvya wa Chadema alimshinda Salum Akilimali aliyekuwa Mgombea kupitia CCM kwa kupata kura 15 dhidi ya 13 za mpinzani wake. Katika kipindi cha upigaji wa kura kuIiibuka mivutano baina ya Madiwani wa Vyama hivyo viwili ambapo CCM walitaka zipigwe kura za siri kwenye eneo maalumu wakati Chadema walikataa wazo hilo na kushinikiza zipigwe kura za siri wakiwa wamekaa kwenye viti vyao bila kuhama.
''Mwenyekiti tunataka kura za siri kwa mujibu wa kanuni za uendeshaji wa vikao vya Madiwani, kwa aina hii ya kukaa hakuna siri yoyote baina yetu Wajumbe, tunaomba sana kanuni za Halmashauri ziheshimiwe' alisema Mbunge wa Kigoma Mjini, Peter Serukamba. Hata hivyo wazo hilo lilikataliwa na Madiwani wa Chadema ambapo lilimalizika kwa kupigiwa kura ambapo Wajumbe 15 walitaka wapige kura wamekaa katika sehemu zao na Wajumbe wengine 13 walishinikiza kura zipigwe katika eneo lililoandaliwa kwa kazi hiyo.
Baada ya kuchaguliwa, Meya huyo mpya alisema katika kipindi chake cha uongozi atahakikisha anadumisha uhusiano na kila mmoja katika kuiendeleza Manispaa hiyo, sambamba na kuwataka Madiwani wasiingize siasa katika kujadili mambo muhimu ya maendeleo. Pia aliwaeleza Watumishi na Watendaji kwamba anayeona hawezi kujituma katika utendaji wa kazi zake, ni bora ahame mapema kabla hajatimuliwa na Vikao halali vya Halmashauri.
''Nawaomba Watendaji, anayeona hawezi kwenda sambamba na kasi hii bora atafute mlango wa kutokea mapema, vinginevyo sitamvumilia yeyote atakayeonekana kuwa kikwazo cha kufikia malengo tuliyojiwekea ambayo ni kuwaletea maendeleo Wananchi wa Manispaa yetu' alisisitiza Beji. mwisho.
Sent from my iPhone

0 comments