Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Arusha kunatisha.. Hali si hali. Mbowe yupo chini ya ulinzi

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Maandamano ya wanaosadikiwa kuwa wanachama na wapenzi wa CHADEMA yakikatisha mitaa ya jiji la Arusha muda mfupi uliopitaPolisi wayapiga stop maandamano hayo
Maandamano yakiwa yamepigwa stop
Maeneo ya unga limited
Arusha hapatoshi dakika hii
MWENYEKITI WA CHADEMA NA MBUNGE WA HAI MH. FREEMAN MBOWE NI MIONGONI MWA VIONGOZI KADHAA WA CHAMA HICHO AMBAO WAKO MIKONONI MWA POLISI JIJINI ARUSHA DAKIKA HII, BAADA YA KUTIWA MBARONI KWA KILE KILICHOONEKANA KUWA MAANDAMANO BATILI.

TIMU YA GLOBU YA JAMII AMBAYO IKO ENEO LA TUKIO LIMEWATAJA VIONGOZI WENGINE WALIO KOROKORONI KUWA NI MBUNGE WA ARUSHA MJINI MH. GODBLESS LEMA, MBUNGE WA ROMBO MH. JOSEPH SELASINI NA WANACHAMA WENGINE KADHAA WA CHADEMA.

HABARI ZINASEMA POLISI WALITAWANYA MAANDAMANO HAYO YALIPOKARIBIA OFISI ZA TAKUKURU NA KWAMBA BAADA YA VUTA NIKUVUTE, MH. MBOWE NA WENZIE WAKAKAMATWA NA KUTUPWA RUMANDE

Habari kutoka Arusha zinasema hali ni tete. Mabomu na risasi za moto zinapigwa ili kutawanya waandamanaji. Hali ya amanai imetoweka kwa muda katika jiji la Arusha. Wafuasi wa Chadema wamekatisha mkutano wa hadhara uliokuwa ukihutubiwa na Dk Slaa. Wafuasi hao wameandamana kuelekea kituo kikuu cha polisi kuwakomboa au kushinikiza kuachiwa kwa viongozi wao. Mbowe, Lema na mpenzi wa DK Slaa wanashikiliwa kituoni hapo. Hatima ya sakata hili huenda ikaacha vifo au majeruhi. tutajua baadae kadri habari zitakavyopatikana.
Tags:

0 comments

Post a Comment