IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Kauli hiyo ilitolewa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema,Zitto Kabwe alipokuwa akihutubia Wananchi wa Kigoma mjini kuelezea mambo mbalimbali yanayohusiana na mustakabali wa kisiasa, ambapo alimshutumu Waziri huyo kwa kutumia Mamlaka yake vibaya.
‘Chadema tuna idadi kubwa ya madiwani zaidi ya CCM, hivyo juhudi zozote zinazofanywa na Waziri kusaidia Chama chake hazitasaidia kitu, badala yake zitaongeza hasira na chuki kwa Wakazi wa Kigoma mjini na kujikuta wakiichukia zaidi CCM na viongozi wake kwa vile anachangia kukwamisha maendeleo ya mji wetu’ alieleza Zitto.
‘Kutokana na hali hiyo, nampa Waziri wa Tamisemi siku saba ahakikishe anaitisha uchaguzi wa kumchagua Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ili tumpate Mwenyekiti wa baraza la madiwani na kamati zake za kudumu waanze kutuhudumia na kusimamia miradi ya maendeleo, kwa sababu kadri Waziri anavyochelewesha uchaguzi ndivyo Watendaji wanavyoweza kutumia vibaya nafasi hiyo kuharibu Halmashauri yetu” aliongeza.
Alisema baada ya uchaguzi Mkuu uliofanyika Oktoba 31 mwaka huu, Chadema walishinda nafasi za madiwani katika Kata 10 dhidi ya tisa walizopata CCM, jambo lililofanya Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutoa nafasi nne za madiwani wa Viti Maalumu wakati CCM walipewa nafasi tatu za Madiwani wa Viti maalumu.
Zitto alisema chanzo cha mgogoro huo ni idadi hiyo ya madiwani wa Viti maalumu ambapo alidai kuwa CCM walikwenda Mahakama ya Wilaya Kigoma kulalamikia mgawo huo, lakini Mahakama ilitupilia mbali shauri hilo.
‘Waziri Mkuchika anapaswa kujua kwamba siku ile alipoandika barua ya kusimamisha uchaguzi wa Meya (Desemba 17, 2010), Mahakama ya Wilaya Kigoma ilikuwa imetoa maamuzi ya shauri la CCM waliotaka Mahakama isimamishe uchaguzi, lakini Hakimu alilitupilia mbali shauri hilo kwa maelezo kwamba Tume ya Uchaguzi ipo sahihi katika mgawanyo wa madiwani wa viti maalumu” alifafanua Zito.
‘Na hata kama Mahakama ingesema okay, CCM waongeongezewa diwani mmoja ili tulingane nao bado wasingekuwa na uwezo wa kushinda halmashauri, labda ile ndoa ya Mseto tuliyofunga nao mwaka 2005 inaonekana wameridhika nayo ndiyo maana wanataka turudiane nao, sisi tunasema kwa hilo hatupo tayari na kamwe mwaka huu hatuipotezi Manispaa ya Kigoma Ujiji’ alisisitiza.
You Are Here: Home - - Zitto atoa siku saba kwa Waziri TAMISEMI
0 comments