Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Zitto ataka kuongoza upinzani bungeni

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter MBUNGE mteule wa Jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ametangaza nia ya kuwania kuwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni katika Bunge la Kumi, nafasi iliyokuwa ikishikiliwa na Hamad Rashid wa CUF kwa miaka mkitano iliyopita.
Akizungumza na Mwananchi jana, Kabwe alisema kuwa anawasiliana na viongozi wa chama chake cha Chadema kuomba apewe ridhaa ya kugombea nafasi hiyo muhimu.

“Niwawasiliana na viongozi wangu kuomba nipewe ridhaa ya kuongoza kambi ya upinzani bungeni... hivi sasa Chadema imepata idadi ya wabunge wa kutosha kuunda kambi ya upinzani,” alisema Zitto.

Alisema kuwa sababu kubwa ya kuwania nafasi hiyo ni kutokana na uzoefu wake bungeni kwa kuwa alishakuwa mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma na pia mjumbe wa Kamati ya Ungozi na kwamba tafiti zote zinaonyesha kuwa yeye ni mbunge bora.
“Nasubiri mwongozo wa chama katika hili,” alisema Zitto.

Akizungumzia suala hilo mshauri wa Chadema, Dk Kitilla Mkumbo alisema: "Zitto kama mbunge ana haki ya kuwania nafasi hiyo na haoni kama kuna tatizo lolote... ni sahihi kufanya hivyo.”
Kuhusu tetesi kuwa nafasi hiyo inawaniwa pia na mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, Dk Mkumbo alisema kuwa hata Mbowe ana haki ya kuwania nafasi hiyo lakini chama ndicho kitatoa maamuzi ya mwisho.
Tags:

0 comments

Post a Comment