Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Waanza kumsaka Meya wa Jiji la Arusha

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter KAMPENI za kumsaka Meya wa jiji la Arusha, zimeanza mjini hapa baada ya kumalizika uchaguzi mkuu na wagombea wa vyama vitatu vya Chadema, CCM na TLP wanatajwa kuwania nafasi hiyo.

Habari za uhakika kutoka ndani ya vyama hivyo, zimebainisha kwamba upande wa Chadema anayetajwa kuwania nafasi hiyo ni Estomii Mallah, CCM Poul loter Laizer na TLP anatajwa Michael Kivuyo kuwania nafasi hiyo.

Hata hivyo, uwezekano wa Kivuyo kupata nafasi hiyo, unaonekana ni mgumu kwani kati ya madiwani wa kuchaguliwa 20, TLP kuna diwani mmoja tu, huku Chadema ikiwa na madiwani tisa pomoja na mbunge na CCM madiwani 10.

Diwani huyo wa TLP hata hivyo kura yake moja ni muhimu katika vyama vyote hatua ambayo sasa inaweza kumfanya awe naibu meya wa jiji hasa kutokana na uzoefu wake wa udiwani kwa miaka 10 sasa.

Hata hivyo, Kama TLP wataunga mkono Chadema, huenda Malla atakuwa Meya wa Jiji la Arusha na na kusababisha Halmashauri ya Jiji kuongozwa na vyama vya upinzani.

Akizungumzia hali hiyo, kiongozi mmoja wa CCM, alisema mpasuko wa viongozi wa CCM wilaya ya Arusha ambao unawagusa baadhi ya madiwani pia huenda ukasababisha, Laizer aliyewahi kuwa Meya kukosa nafasi hiyo.

Hakuna kiongozi wa Chadema au TLP ambao walikubali kwa sasa kutoa maoni yao kuhusiana na mchakato wa Meya kwa maelezo kuwa jambo hilo bado linafanyiwa kazi ndani ya vyama hivyo.

"Ni mapema mno leo kusema tutashinda nafasi ya Umeya kwani sisi Chadema tunahitaji kura ya TLP na CCM pia ili kujihakikishia nafasi hiyo na hata CCM nao wanahitaji kura zetu na TLP," alisema diwani mmoja wa Chadema ambaye aliomba kutotajwa jina kwa sasa.
Tags:

0 comments

Post a Comment