Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Uingereza yasema suala la Chenge litaisha mahakani tuu

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Andrew Chenge


SIKU mbili baada ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kutoa taarifa ya kumsafisha Andrew Chenge dhidi ya kashfa ya rada, Serikali ya Uingereza imesema suala hilo halijaisha wala kufungwa.

Taarifa hiyo iliyosambazwa jana kwenye vyombo vya habari imesema ni mapema mno kusema wahusika wa kashfa ya rada hawana hatia kwa vile kesi hiyo haijafikishwa mahakamani.

Novemba 8 mwaka huu Takukuru iliwasha upya moto kashfa ya ununuzi wa rada baada ya kutoa taarifa inayoeleza kuwa Chenge ambaye alikuwa Mwanasheria Mkuu wa serikali wakati wa Serikali ya Awamu ya Tatu, hakuhusika kwenye kashfa ya ununuzi wa rada.

Takukuru ilitoa taarifa hiyo siku moja baada ya Chenge ambaye ni mbunge mteule wa Bariadi Magharibi, kiutisha mkutano wa waandishi na kutamba kuwa hahusiki na kashfa ya rada.

Taarifa yaTakukuru kumsafisha Chenge ilitolewa baada ya kutangaza kuwania kiti cha Spika wa Bunge la Jamhuri na kuuponda uongozi wa Sitta kwa ulisababisha makundi na chuki ndani ya Bunge.


Lakini Serikali ya Uingereza ilisema katika taarifa iliyotolewa na ubalozi wake nchini jana kuwa taarifa hiyo ya Takukuru sio sahihi, kwani suala hilo halijafikishwa mahakamani.

"Wakati huu kesi inayoihusu kampuni ya BAe na wahusika wake nchini Tanzania, haijafikishwa mahakamani. Kwa hiyo haiwezekani kuhitimisha suala hilo kwa namna yeyote ile ikiwamo kuwaondoa wahusika waliohojiwa na SFO," ilisema taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilifafanua kuwa Februari 5 mwaka huu, SFO ilitangaza kuwa imefikia mwafaka na kampuni ya BAe katika uchunguzi wake wa mkataba wa ununuzi wa rada hiyo na serikali ya Tanzania.


"BAE ilikiri kuwa imeshindwa kuweka rekodi sahihi za kihasibu katika uendeshaji wa shughuli zake hapa nchini. Hivyo ilikiri kosa na kukubali kulipa Paundi 30 milioni kama faini na fidia kwa serikali ya Tanzania," ilisema taarifa hiyo.

Lakini, taarifa hiyo ikaongeza kuwa Mahakama Kuu ya Uingereza ambayo itaanza kusikiliza kesi hiyo ya rada Novemba 23 mwaka huu, ndio yenye mamlaka ya kupanga kiasi cha faini na fidia inayopaswa kulipwa na kampuni ya BAE.

"Makubaliano hayo kati ya SFO na BAE ndiyo yaliyohitimisha uchunguzi wa taasisi hiyo ya makosa makubwa ya jinai dhidi ya suala hilo la rada," ilisema taarifa hiyo na kuongeza:

"Lakini kwa kuwa makubaliano hayo hayajathibitishwa na Mahakama, sio sahihi kusema sasa kwamba, suala hilo limemalizika."
Tags:

0 comments

Post a Comment