Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - MARANDO KUGOMBEA USPIKA

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Mabere Marando.



Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimempendekeza wakili maarufu ambaye pia ni mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho, Mabere Nyaucho Marando (pichani), kugombea nafasi ya spika wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Taarifa zilizopatikana kutoka vyanzo vyetu vya habari ndani ya Chadema zinasema chama hicho kimeamua kumpendekeza Marando kuchuana na wagombea wa nafasi hiyo kutoka katika vyama vingine watakaoteuliwa kuwania nafasi hiyo.

Marando alipopigiwa simu na mwandishi wetu na kuulizwa kuhusu kuchaguliwa kwake kugombea nafasi hiyo nyeti, alikiri na kusema yupo tayari kuchuana na wagombea wengine na anaamini ataibuka na ushindi.

“Nikichaguliwa na wabunge nitahakikisha tunaipitia upya katiba ya nchi na naamini nitabadilisha sura ya bunge letu tukufu,” alisema.

Marando amewahi kuwa Mbunge wa Jimbo la Rorya kupitia chama cha NCCR-Mageuzi na baadaye akawa Mbunge wa Tanzania katika Bunge la Afrika Mashariki Baadhi ya watu maarufu waliojitokeza kugombea nafasi hiyo kutoka Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni spika aliyemaliza muda wake, Samuel Sitta, Andrew Chenge, Kate Kamba na Job Ndugai. Hata hivyo, vyama vingine havijatangaza wanachama wao wanaowania nafasi hiyo.
Tags:

0 comments

Post a Comment