Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - uchaguzi wa Tanzania Takwimu kwa Hisani ya BBC

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Taarifa na takwimu uchaguzi wa Tanzania

Watanzania wataelekea vituo vya kupiga kura ifikapo tarehe 31 Oktoba 2010. Uchaguzi huu ni muhimu kwa nchi hiyo hasa kwa kuwa chama tawala hakijawahi kutolewa madarakani tangu ilipopata uhuru mwaka 1961. Yafuatayo ni baadhi ya maswala muhimu yanayohusu uchaguzi wa Tanzania 2010.
Tanzania ina idadi kubwa kiasi gani ya wakazi?
Kwa mujibu wa Benki ya Dunia takwimu za mwaka 2008, Tanzania ina wakazi wapatao milioni 42. Umoja wa Mataifa ulikadiria mwaka 2009 kuwa Tanzania ilikuwa na wakazi milioni 43.7.
Watu wangapi wamejiandikisha kupiga kura?
Tume ya uchaguzi ya Tanzania imetangaza kuwa watu waliojiandikisha kupiga kura ni milioni 19.
Je watanzania watapiga kura siku gani?
Siku ya kupiga kura ni tarehe 31 Oktoba 2010
Kampeni zilianza lini na zitaisha lini?
Kampeni za uchaguzi wa Tanzania zilianza Agosti 31, na mwisho wa kampeni ni tarehe 30 Oktoba 2010.
Kuna wagombea wangapi wa kiti cha Rais?
Kwa kiti cha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuna wagombea saba, vile katika uchaguzi wa Rais wa Zanzibar kuna wagombea sita.
Tanzania ina majimbo mangapi ya uchaguzi?
Kwa Tanzania na Bara na Zanziba kuna jumla ya majimbo ya ubunge 239
Je Rais na wabunge hukaa madarakani kwa miaka mingapi?
Kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, Rais huchaguliwa na kuwepo madarakani kwa muda wa miaka mitano kabla ya uchaguzi mwingine kufanyika. Sheria hiyo hutumika kwa wabunge na madiwani.
Jina kamili ni nini?
Nchi hii hutambulika kama Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa shughuli rasmi.
Je Tanzania ukubwa wa nchi kiasi gani?
Tanzania ina ukubwa wa kilometa za mraba 945,087.
Lugha Rasmi ni zipi?
Lugha zinazotumika kwa shughuli rasmi ni Kiingereza na Kiswahili.
Dini kubwa ni zipi?
Ingawa kuna dini nyingine ndogo ndogo, idadi kubwa ya watanzania ni wakristu na waislamu.
Tags:

0 comments

Post a Comment