Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Kifo cha Mgombea Kutokea? kiwewe chatanda

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Na Issa Mnally
Hali ya Mgombea Mwenza wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya NCCR-Mageuzi, Ali Omar Juma ikielezwa inarejea vizuri, kiwewe kinatawala kuhusu anayetajwa kufariki dunia kabla ya Uchaguzi Mkuu Oktoba 31, 2010.

Ingawa wagombea wenyewe hawaoneshi kutetereka kwa namna yoyote kutokana na tishio la mmoja wao kufariki dunia, lakini uchunguzi unaonesha kuwa swali la ‘nani atakufa’ linasumbua ubongo.
Dk. Slaa (CHADEMA)
Tayari imekwisharipotiwa kwamba baadhi ya Watanzania walikata tamaa mapema, tangu waliposikia utabiri kuwa mwaka huu hakutakuwa na Uchaguzi Mkuu kwa sababu mmoja wa Wagombea Urais mwenye nguvu atafariki.

Mnajimu alwatan barani Afrika, Sheikh Yahya Hussein ndiye sababu ya sakata hilo kupitia utabiri wake na katika mazungumzo na gazeti hili Ijumaa iliyopita alisisitiza kwamba siku zimebaki chache lakini mgombea mmoja ataaga dunia.

Sheikh Yahya aliliambia Ijumaa Wikienda ‘The Biggest IQ Paper’ kuwa ni lazima Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) ijiandae kuhairisha uchaguzi kwa sababu macho yake yameona na yana uthibitisho wa kifo cha mmoja wa wagombea.
Hashim Rungwe (NCCR-MAGEUZI)
Alisema, anachokifanya yeye ni kutabiri kwa kufasiri nyota lakini siyo uchawi kama ambavyo wengi wamekuwa wakiamini.

“Huu ni utabiri siyo uchawi, siku bado zipo, kwahiyo tungoje siku kati ya hizi chache zilizobaki, yatatimia tu niliyoyasema,” alisema Sheikh Yahya.

Katika hatua nyingine, wananchi mbalimbali waliozungumza na gazeti hili walisema kuwa utabiri wa Sheikh Yahya ni mtihani kwa taifa kwa sababu ngoja ngoja inatia kiwewe.

“Sisi wananchi tunawaza sana, labda nisiwasemee watu nijiseme mimi mwenyewe, nina mawazo mengi kusema kweli,” alisema Faustine Kimadao wa Boko, Dar es Salaam katika mahojiano yaliyofanyika Kituo cha Daladala, Mwenge.

Kimadao alisema: “Watu ambao tunaamini katika siasa, hii inatugusa sana, tunaweza kudharau ya Sheikh Yahya lakini tukumbuke kwamba mwaka 2005 alitabiri na ikatokea.
Jakaya Kikwete (CCM)
“Alisema Rais Mkapa (Benjamin) ataongezewa muda wa kutawala kwa sababu uchaguzi utaahirishwa na kweli ikatokea. Tuyatazame haya katika pande mbili, binafsi nina hofu.”

Mtanzania mwingine, Bora Steven katika mahojiano hayo alisema kuwa mwanzoni alikuwa anapuuzia lakini siku zinavyokaribia anaanza kupata mchecheto kwa sababu kuna alama za huzuni.

“Kwa vyovyote vile, mgombea yoyote wa Urais akifariki ni maumivu kwa taifa, kwa kuanzia kuangalia chama chake, wafuasi na gharama ambazo nchi itaingia baada ya uchaguzi kuhairishwa,” alisema Bora.

Aliongeza: “Tunamuomba Mungu atuepushie kwa sababu Sheikh Yahya ametabiri tu lakini mwisho wa siku, Mungu ana nafasi kubwa ya kuamua kinyume chake.”
Ibrahim Lipumba (CUF)
Maoni zaidi
Khatib Mitea, muuza mafuta, alisema: “Mimi kwa mtazamo wangu Sheikh Yahya katabiri lakini akumbuke kuwa yeye sio Mungu, sidhani kama itatokea kwa mtazamo.”

Salum Nassor, dereva taksi alisema: “Sheikh ni haki yake kutabiri lakini atambue kuwa Dini ya Kiislamu inasema utabiri ni dhambi, mimi nawafuatilia sana hawa wagombea wa Urais mpaka sasa sidhani kama kuna mgombea atakufa.”

Majaliwa Robert, muuza vocha Bamaga, Mwenge: “Mimi kwa upande wangu namwamini sana Sheikh Yahya, nawataka Watanzania wakae chonjo. Unakumbuka mwaka 2005 alitabiri uchaguzi utahairishwa na ukahairishwa kweli.”

Khatibu Idd, alisema: “Siwezi kuamini kama mmoja wa Wagombea wa Urais atapoteza maisha, kwa mtazamo wangu yule mtabiri alikuwa anawatisha tu Watanzania wasijitokeze kuchukua fomu.”
Mugahywa Muttamwega (TLP)
Thomas Maganga: “Mimi sipendi sana kuamini mambo hayo ya utabiri, lakini yule Sheikh ni mtabiri wa Kimataifa nawataka Watanzania wenzagu tusubiri tuone kile kitakacho tokea.”

Upande mwingine, baadhi ya wananchi wameeleza hofu yao kwamba kuna uwezekano mkubwa kwa Freemasons kuichagulia Tanzania Rais.

“Tunasikia Freemasons wakimtaka mtu fulani ndiye ashinde Urais basi atashinda na yule wasiyemtaka hatapata kitu, kwahiyo tunaogopa hilo,” alisema Halima Jaffar wa Ubungo, Dar.

Mkazi wa Kinondoni, Jadu Kitani alisema kuwa tishio kwamba nchi nyingi marais ni Freemasons ndiyo linafanya ahisi wanaweza wakasimika mtu wao Tanzania.
Peter Kuga Mziray (APPT-MAENDELEO) 
“Mimi sijui kama kuna mgombea yoyote wa Urais ni Fraemason lakini najua wanataka kuitawala dunia, kwahiyo inawezekana kabisa wameandaa mtu wao. Mungu asaidie washindwe,” alisema Jadu.
Tags:

0 comments

Post a Comment