Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Sasa Gongo maarufu kama changaa ruksa Kenya

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter Kibaki haruhusu unywaji wa chang'aa Kenya Send to a friend
Thursday, 02 September 2010 22:08

MWANDISHI WA MWANANCHI, Nairobi

WALEVI wa chang'aa na pombe nyingine za bei rahisi sasa watabugia pombe bila ya hofu ya kukamatwa, baada ya Rais Mwai Kibaki kuidhinisha Mswada wa Pombe uwe sheria.

Habari zinasema kuwa katika tangazo la gazeti rasmi la Serikali, Rais Kibaki aliufanya sheria mswada huo uliowasilishwa bungeni na Mbunge wa Naivasha John Mututho na kupitishwa na bunge mnamo Juni.

Sheria hiyo sasa inazipatia kampuni za pombe miezi sita kuanza kutengeza pombe za kiwango cha chini kama vile chang'aa na kupunguza bei za pombe hizo, ili mwananchi wa pato la chini aweze kuzinunua.

Kwa mujibu wa sheria hiyo, pombe hizo ambazo zimekuwa zikitengnezwa na kuhifadhiwa katika mazingira duni sasa zitakuwa zikifungwa kwenye pakiti zitakazozifanya salama kwa wanywaji.
Sheria hiyo inasema, "Chang'aa itaruhusiwa tu ikiwa itatengezwa na kufungwa au kuuzwa ikiwa kwenye glasi."

Kwa hivyo, ijapokuwa utengezaji na uuzaji wa chang'aa umeidhinishwa, ni watu watakaozingatia kanuni hizo pekee watakaoruhusiwa kuendeleza biashara.

Hata hivyo, huenda sheria hii ikakumbwa na malalamiko, hasa kutoka kwa viongozi wa kidini, ikizingatiwa kuwa pombe hizo za kienyeji zimekuwa chanzo cha vifo vya mamia ya watu tangu mwaka huu uanze.

Mwanzoni mwa mwaka huu, watu kadhaa walifariki katika mtaa wa Shauri Moyo jijini Nairobi kabla ya wengine 17 kufariki mnamo Julai kwa kunywa pombe zilizochanganywa na kemikali hatari.
Tags:

0 comments

Post a Comment