Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Marekani na Urusi yabadilishana mawakala wa ujasusi

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Marekani na Urusi yabadilishana mawakala wa ujasusi

 

Urusi na Marekani zimetekeleza mabadilishano makubwa ya majasusi tangu kumalizika kwa vita baridi, yaliyofanyika katika uwanja wa ndege wa Vienna , nchini Austria.

 
Moscow.
Urusi  na  Marekani  zimetekeleza  mabadilishano makubwa  ya  majasusi  tangu   kumalizika  kwa  vita baridi,  yaliyofanyika  katika  uwanja  wa  ndege  wa Vienna, nchini  Austria. Ndege  moja  iliwaleta  mawakala 10  wa  Urusi  walioachiwa  kutoka  Marekani   baada  ya kikao  cha  mahakama , ambapo  walikiri  kufanya  upelelezi wa  kijasusi. Ndege  nyingine  iliripotiwa  kuwa  na  watu wanne  ambao  walihukumiwa  kufanya  ujasusi  nchini Urusi, ambao  wamepewa  msamaha  wa  rais  baada  ya kutia  saini  taarifa   kuwa  wana  hatia. Mmoja  kati  ya wale  waliohusika  katika  ubadilishanaji  huo, ni  mtaalamu wa  masuala  ya  kinuklia  Igor Sutyagin  ambaye  alifungwa jela   nchini  Urusi  mwaka  2004. Kaka  yake  Dmitry amesema   kuwa  Igor  atawasili  nyumbani   hivi  karibuni. Tukio  lote  hilo  limekamilika   haraka ,  hali  inayoashiria kuwa  Urusi  na  Marekani  zote  zina  nia  ya  kuepusha athari  katika  uhusiano  wao.
Tags:

0 comments

Post a Comment