Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Mgahywa wa TLP kuwania urais

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter MBUNGE wa zamani wa Mwibara kwa tiketi ya Mutamwega Mgahywa ametangaza nia yake ya kugombea urais kwa tiketi ya TLP katika uchaguzi mkuu ujao.

Mgahywa alitangaza jana Dar es Salaam mbele ya waandishi wa habari na wanachama wenzake.

“Nilianza siasa mwaka 1989 na leo nina miaka 42, kwa mujibu wa sheria mgombea urais anatakiwa kuwa na umri kuanzia miaka 40 na mimi ninayo, nikiwa Mtanzania nimeona ninastahili kuwatumikia wananchi, na leo nimekuja kutoa azma yangu na wananchi wakinihitaji niko tayari kuwatumikia,” alisema.

Mgahywa ambaye ni mwanachama hai wa TLP na alikuwa mbunge wa Mwibara miaka 10 kuanzia 1995 hadi 2005, alisema akiwa na uzoefu huo wa ubunge na miaka 20 katika siasa, anaamini anaweza kuibadilisha Tanzania kwa kushirikiana na wananchi.

“Tukishirikiana Watanzania wote tunaweza kuleta mabadiliko. Naamini naweza kuunda Serikali itakayorudisha heshima kwa nchi hii, huo ni mtazamo wangu katika nafsi yangu … siku ya kuchukua fomu nitawaita tena niwaeleze kwa undani mikakati yangu … nchi hii ni ya wote si ya Juma wala John,” alisema.

Alitoa mwito kwa mwenye uwezo au nia, asisite kujitokeza na kuingia katika ulingo wa siasa na kuongeza kuwa milango iko wazi kwa anayetaka kushiriki kinyang’anyiro hicho.

Katibu Mkuu wa TLP, Jesse Makundi, alisema kunzia jana TLP inatangaza rasmi nafasi ya ugombea urais iko wazi kwa yeyote atakayejisikia kuchukua fomu na mwisho wa kurudisha ni Julai 30 mwaka huu.

Makundi alisema baada ya Mwenyekiti wa TLP, Augustine Mrema, kutangaza kugombea ubunge wa Vunjo nafasi ya mgombea urais kwa tiketi ya chama hicho ilikuwa wazi, kwani miaka yote Mrema alikuwa akijitokeza.

“Sasa ni wakati muafaka kwa Watanzania kujua kuwa nafasi ziko wazi kwa Mtanzania yeyote atakayetaka kugombea nafasi hiyo kupitia tiketi ya TLP,” alisema Makundi.
Tags:

0 comments

Post a Comment