IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Akiitaja mikoa ambayo viongozi hao walitiwa mbaroni na kuwekwa ndani, Mtatiro alisema kuwa ni pamoja na Dar es Salaam (5), Pwani (5), Morogoro (2), Tanga (58), Dodoma (2), Tabora (8), Singida (2) na Kagera (6).
Mikoa mingine ni Kigoma (1), Lindi (6), Mara (5), Mtwara (10), Mwanza (11), Rukwa (1), Ruvuma (4), Shinyanga (12) ambao jumla yake ni viongozi 138.
HOMA ya uchaguzi imeanza kupanda kufuatia Chama Cha Wananchi(CUF), kuwatuhumu jeshi la Polisi, kikidai kwamba wameanza kutekeleza kauli mbiu ya ‘Ushindi ni Lazima 2010’, iliyozinduliwa na Chama cha Mapinduzi(CCM) kufuatia kukamatwa jumla ya viongozi 138 wa mitaa, vijiji na vitongoji, tuhuma ambazo hazikufafanuliwa na jeshi hilo.
CCM ilizindua kauli mbiu hiyo hivi karibuni katika ukumbi wa Mlimani City sanjari na uzinduzi wa programu maalumu ya harambee ya kutunisha mfuko wa uchaguzi wa chama hicho kwa njia ya mtandao ambao, unahitaji jumla ya Sh40 bilioni.
Akizungumza na waandishi wa habari katika makao makuu ya CUF Buguruni jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa Haki za Binadamu na Sheria wa chama hicho, Julius Mtatiro, alisema Polisi na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) wanahusika moja kwa moja katika kufanikisha kauli mbiu hiyo ya CCM.
“Kwa nini viongozi wetu 138 ambao ni wenyeviti wa mitaa, vijiji na vitongoji tunaowategemea katika kuimarisha chama katika maeneo yao wakamatwe na kuwekwa ndani na kubambikiziwa kesi za jinai, ambazo hata dhamana hupati?,”alisema.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, John Chiligati alisema CUF haina ushahidi juu ya hayo na kwamba inajisemea tu kutokana na homa yao ya uchaguzi.
“Mimi nadhani ni homa ya uchaguzi tu, naamini wanajisemea kwa sababu Polisi wana taratibu, sheria, kanuni na miongozo yao katika kufanya kazi zao,” alisema Chiligati.
“Polisi wakitaka kumkamata mtu hawamuulizi kabila, rangi wala dini, hata ukienda huko magerezani au mahubusu hata CCM wako wengi, hii ni kwa sababu uhalifu hauna itikadi, rangi, kabila wala dini.”
Naye Msemaji wa Polisi, Abdallah Msika alipolizungumzia suala hilo alisema hana majibu ya tuhuma hizo kwa sasa hadi hapo atakapokutana na viongozi wenzake wa polisi.
“Sijui nijibu nini kwa sasa, kwani wewe ndio unanipa taarifa, ni vema ukaandika maswali yako ukaleta hapa ofisini kesho (leo), halafu tukayapeleke kwa viongozi ili upate majibu yake,” alisema Msika.
“Kwa sababu msemaji si papo kwa hapo kama ulivyouliza, wewe andika maswali, ulete hapa, halafu tutakujibu,”.
Kwa upande wa Mtatiro alisema baadhi ya viongozi waliokamatwa walikuwa wanategemewa majimboni kwao kugombea nafasi mbalimbali za uongozi zikiwamo za ubunge na udiwani katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 30 mwaka huu nchini kote.
“Tangu ufanyike uchaguzi wa serikali za mitaa, vijiji na vitongoji Oktoba mwaka jana, kumekuwa na mfululizo wa matukio ya kukamatwa kwa viongozi wetu wa vijiji, mitaa na vitongoji walioshinda katika uchaguzi huo,” alisema Mtatiro.
Kwa mujibu wa Mtatiro mikoa ya Tanga, Shinyanga, Mwanza, Mtwara na Tabora inaongoza kwa kukamatwa viongozi hao kwa wingi
You Are Here: Home - - CUF waishushia Polisi tuhuma nzito za kuwakamata viongozi wa CUF
0 comments