Hatua ya kupindua serikali ilitokea jana kufuatia maandamano makubwa na ghasia zilizokumba taifa hilo la bara Asia.
Viongozi hao hasa wanamsaka Rais Kurmanbek Bakiyev, ambaye wanasema anajaribu kukandamiza upinzani.
Aidha viongozi hao wamesema watasalia madarakani kwa muda wa miezi sita ili kuweza kuudwa katiba mpya. .
Hata hivyo Kiongozi wa serikali ya mda Roza Otunbayeva amemtaka rais Bakiyev ajiuzulu.


0 comments