Viongozi wakuu wa kanisa Katoliki na wengine kutoka makanisa ya Protestanti nchini Ireland wamemkosoa mkuu wa kiongozi wa kanisa Anglikana duniani kwa matamshi aliyoyatoa akisema kanisa katoliki limepoteza heshima yake yote kutokana na kashfa za watoto kunyanyaswa kimapenzi.
Askofu mkuu wa kanisa katoloki mjini Dublin, Diarmuid Martin, amesema ameshangazwa na kuvunjwa moyo na matamshi hayo ya kwanza ya kiongozi wa kanisa Anglikana duniani Dr Rowan Williams kuhusu kashfa hiyo.
Dr Williams ameshampigia simu Askofu Martin kuelezea huzuni yake na kujuta kwa uchungu ambao matamshi yake yanaweza kuwa yalisababisha, na kusema hakuwa na nia ya kukosea au kukosoa kanisa nchini Ireland.
0 comments