Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Dakika tatu zaishusha Prisons, Manyema yafia Tanga, yaifuata Moro

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter BAO lililofungwa na Steve Bengo wa Yanga katika dakika ya 87, lilitosha kuishusha Prisons ya Mbeya Daraja la Kwanza, baada ya miaka 15 katika mchezo wa kufunga pazia wa Ligi Kuu uliofayika kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya.

Prisons iliyotoka sare ya 1-1 na Yanga, sasa inaungana na Moro United na Manyema kushuka daraja na sasa zitacheza Ligi Daraja la Kwanza msimu ujao.

Nafasi za timu hizo zimeshazibwa na AFC Arusha, Polisi Dodoma na Ruvu Shooting zilizopanda Ligi Kuu msimu ujao baada ya kushika nafasi tatu za juu, michuano iliyofanyika mkoani Arusha.

Prisons ilikuwa iokoke kama ingeifunga Yanga, lakini dakika tatu, zilitosha kuimaliza timu hiyo baada ya kuongoza kwa bao la Sospeter Wenga aliyefunga bao dakika ya 70 ikiwa ni dakika 10 baada ya mchezaji wa Prisons, Fred Chudu kutolewa kwa kadi nyekundu.

Kwa upande wa Manyema iliyotoka suluhu jana, ilikuwa ikihitaji ushindi tu dhidi ya Azam iweze kukwepa kushuka, kwani ingefikisha pointi 25 ambazo ni zaidi ya Majimaji na Kagera zilizomaliza zikiwa na pointi 24.

Ukiacha timu hizo zilizoshuka, Simba imeweka rekodi ya aina yake msimu huu baada ya kumaliza ligi kwa kishindo kwa kuizabua Mtibwa Sugar ya Morogoro mabao 4-0 katika mchezo mkali uliofanyika kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Simba imetwaa ubingwa mwaka huu kwa kufikisha pointi 62 ikiwa haijapoteza hata mchezo mmoja huku ikiwa imefunga mabao 50 na kufikisha pointi 62. Yanga ni ya pili baada ya kufikisha pointi 49.

Mshambuliaji wa Simba Mussa Hassan Mgosi ameibuka mfungaji bora kwa kupachika mabao 18 sawa na mfungaji bora wa msimu uliopita, Boniface Ambani.

Timu zilizosalimika ni Azam FC na African Lyon ya Dar es Salaam, Mtibwa Sugar ya Morogoro, JKT Ruvu ya Pwani, Toto African ya Mwanza, Majimaji ya Songea na Kagera Sugar ya Kagera.
Tags:

0 comments

Post a Comment