IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
UONGOZI Simba umedai kuhujumiwa na watani wao Yanga kufuatia taarifa za wachezaji wake Emmanuel Okwi na Joseph Owino kudaiwa kutoweka kambini.
Gazeti moja la michezo linalotoka Jumatano (jina tunalo) liliandika juzi kwamba wachezaji hao wako mbioni kuhamia Yanga.
Akizungumza na waandishi wa Habari Dar es Salaam jana, Ofisa habari wa Simba, Cliford Ndimbo alisema wanahisi taarifa hiyo iliyotolewa na gazeti hilo ina lengo la kuwahujumu kwa kushirikiana na Yanga.
Simba na Yanga zinatarajiwa kumenyana Aprili 11 katika mechi ya Ligi Kuu itakayochezwa kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Ndimbo alisema, kuwa habari hiyo inawagawa wachezaji wa timu yake ambao wanajiandaa na mechi ya Kombe la Shirikisho dhidi ya Lengthens ya Zimbabwe itakayochezwa Aprili 4 kwenye Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam.
Ndimbo alisema kuwa kwa jinsi habari hiyo ilivyoandika ineonekana kana kwamba tayari makubaliano yamefikiwa kuhusiana na kuhama kwa wachezaji hao kitu ambacho si sahihi.
Aidha Ndimbo alisema tayari wameandika barua ya malalamiko kwa Baraza la Habari Tanzania (MCT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)
Ndimbo alisema kuwa jana ilikuwa siku ya mwisho kwa wachezaji wa kigeni kuwasili kambini ambapo alisema anaimani hata Owini na Okwi nao watakuwepo.
Lakini habari zingine zilizopatikana jana zilidai kuwa Okwi na mwenzake aalitoroka kambini tangu timu ilipoenda Zimbabwe kucheza na Lengthen.
Alipoulizwa habari hizo Mwenyekiti wa Yanga Imani Madega alipinga na kusema kwamba wao wanafuata taratibu za usajili na hawawezi kuzikiuka.
You Are Here: Home - HABARI ZA MICHEZO - Yanga inatuhuhujumu – Simba
0 comments