Serikali ya Sudan imezindua mtandao wa reli unaounganisha Kaskazini na Kusini mwa nchi hiyo, kwa mara ya kwanza tangu mapigano ya wenyewe kwa wenyewe kuzuka.
Reli hiyo inaunganisha mji wa Babanusa katikati mwa nchi hiyo na mji wa Wau Kusini mwa nchi hiyo. Maafisa wa serikali wanasema reli hiyo itaimarisha uhusiano wa kibiashara na kupunguza gharama za kusafirisha mizigo.
Inakisiwa kuwa zaidi ya watu milioni mbili waliuawa wengi wao wakiwa rais wa Kusini mwa nchi hiyo wakati wa vita hivyo vya wenyewe kwa wenywe vilivyomalizika mwaka wa 2005.
0 comments