Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Israel yakosolewa vikali na waziri Clinton

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton ametoa matamshi mapya makali huku mvutano ukizidi kati ya Marekani na Israel kuhusu mpango wa kujenga makaazi mapya ya Wayahudi katika Jerusalem ya Mashariki iliyoikalia. Amesema, ni tusi kwa Israel kutangaza mpango huo wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Marekani Joe Biden.
Hapo awali, Clinton alizungumza kwa simu na Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu kwa dakika 43, kupinga vikali hatua iliyochukuliwa na Israel.Amesema, hatua ya Israel imedhoofisha jitahada za Marekani za kutaka kuanzisha majadiliano mapya ya amani.
O-TON: CLINTON
Waziri Clinton anasema,"Jumuiya ya kimataifa lazima iwe na msimamo imara wa pamoja kuunga mkono suluhisho la mataifa mawili."
Hata kundi la pande nne linaloshughulikia majadiliano ya amani ya Mashariki ya Kati limeikosoa Israel kwa kile kilichoitwa mipango yake ya uchokozi ya kutaka kujenga makaazi mapya ya Wayahudi.Kundi la pande nne linajumuisha Marekani,Umoja wa Mataifa,Umoja wa Ulaya na Urusi. Wajumbe wake wamesema mpango wa Israel utajadiliwa katika mkutano wao mjini Moscow,uliopangwa tangu hapo awali. Serikali ya Israel imesema tangazo lake lilikuwa kosa la urasimu.
Tags:

0 comments

Post a Comment