Serikali ya Haiti imewatia kizuizini Wamarekani kumi ambao inasema walikuwa wakijaribu kuwasafirisha nje ya nchi watoto wadogo bila idhini ya serikali.
Msemaji wa serikali ya Haiti, Yves Christallin, alisema Wamarekani hao walikamatwa na zaidi ya watoto thelathini kwenye mpaka na Jamhuri ya Dominica, ambako walisema walikuwa na kituo cha watoto yatima.
Msemaji huyo alisema Wamarekani hao hawakuwa na hati zinazothibitisha ikiwa watoto hao walikuwa ni yatima kutokana na tetemeko la ardhi lililoikumba Haiti hivi karibuni.
Wamarekani hao ni kutoka kanisa lenye makao yake katika jimbo la Idaho.
Mchungaji katika kanisa hilo, Clint Henry ameiambia BBC kuwa kundi hilo la Wamarekani limekuwa na hati zote zinazohitajika kufanya shughuli zao.
0 comments