Raia 12 wa Afghanistan wameuawa kimakosa kwenye operesheni inayofanywa na vikosi vya jumuiya ya kujihami ya NATO kusini mwa nchi hiyo. Maroketi mawili yaliyofyetuliwa na wanajeshi wa NATO kuwalenga wanamgambo wa Taliban waliokuwa wakiwashambulia kwa risasi, yamewakosa wapiganaji hao na badala yake kuanguka kwenye nyumba moja na kuwaua watu 12.
Rais wa Afghanistan Hamid Karzai ameelezea masikito yake makubwa akisema wahanga hao ni jamaa wa familia moja na ametaka kufanyike uchunguzi. Kamanda wa jeshi la NATO nchini Afghanitan, Jenerali Stanley McCrystal amemuomba radhi rais Karzai na kusema matumizi ya maroketi ya aina hiyo yamesitishwa kusubiri uchunguzi ufanyike.
Jeshi la NATO linafanya harakati kubwa kuwahi kufanywa dhidi ya mojawapo ya ngome za wapiganaji wa Taliban katika mji wa Marjah kusini mwa Afghanistan.
0 comments