Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Marekani yatuhumiwa kuchochea vita

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter

Kiongozi mkuu wa kidini nchini Iran Ayatollah Ali Khamanei hii leo akijibu shutuma za Marekani kuwa Iran inaelekea kwenye udikteta wa kijeshi,ameituhumu Marekani kuwa inachochea vita.

Matamshi ya Ayatollah Ali Khamenei ni ishara mpya ya mivutano inayozidi kuongezeka kati ya Tehran na Washington kuhusiana na mradi wa nyuklia wa Iran unaohofiwa na nchi za Magharibi kuwa unalenga kutengeneza silaha za nyuklia. Akiashiria ziara iliyofanywa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Hillary Clinton mapema juma hili katika Mashariki ya Kati, Khamenei amesema kuwa Marekani imemtuma wakala wake katika kanda hiyo kuishutumu serikali ya Iran iliyo na mfumo wa Kiislamu. Lakini hakuna anaeamini uongo unaoenezwa kwani wanafahamu kuwa Marekani ni mchochea vita na kuongezea kuwa eneo la Ghuba limefanywa ghala ya silaha. Wamezivamia Afghanistan na Iraq na sasa wanaituhumu Jamhuri ya Kiislamu amesema kiongozi mkuu wa kidini wa Iran. Secretary of State Hillary Rodham Clinton speaks during her joint news conference with Yemen's Foreign Minister Abu Bakr al-Qirbi, not shown, Thursday, Jan. 21, 2010,  at the State Department in Washington. (AP Photo/Luis M. Alvarez)Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, Hillary Clinton.Lakini mapema wiki hii, Clinton alipokuwa ziarani nchini Qatar na Saudi Arabia alikanusha kuwa Marekani ina njama ya kuishambulia Iran. Amesema, Washington inataka kujadiliana na Tehran lakini haiwezi kubakia kimya wakati Iran ikiendelea na mpango unaoshukiwa kuhusika na silaha za nyuklia. Nchi za magharibi zinapaza sauti kuiwekea Iran vikwazo vipya hasa baada ya Rais Mahmoud Ahmedinejad juma lililopita kutoa amri ya kuanza kusafisha madini ya uranium kwa kiwango cha juu. Marekani inashika bendera katika kulihimiza Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa liweke vikwazo ziada dhidi ya Iran. Lakini Iran inashikilia kuwa azma ya mradi wake wa nyuklia ni kupata umeme zaidi ili iweze kusafirisha mafuta na gesi zaidi kutoka nchi hiyo. Ikisisitiza kuwa mpango wake wa nyuklia ni kwa matumizi ya amani tu,vile vile imeonya kuwa itajibu shambulio lo lote litakalofanywa dhidi yake. Mwezi uliopita, maafisa wa Marekani walisema kuwa Washington imeimarisha mfumo wake wa ulinzi kwenye nchi kavu na baharini katika eneo la Ghuba ili iweze kukabiliana na kile kinachotazamwa kama kitisho kinachozidi kuwa kikubwa kuhusu makombora ya Iran. Eneo hilo la Ghuba ni muhimu kwa usafirishaji wa mafuta duniani. Kwa upande mwingine, vyombo vya habari nchini Urusi vimemnukulu Mnadhimu Mkuu wa nchi hiyo, Jemadari Nikolai Makarov akidai kuwa Marekani inadhamiria kuishambulia Iran. Yeye amenukuliwa akisema kuwa mwenyekiti wa majeshi ya Marekani, Admeri Michael Mullen, hivi karibuni alizungumzia mpango huo. Mwandishi: Martin,Prema/ RTRE/APE Mhariri: Abdul-Rahman,Mohammed

Tags:

0 comments

Post a Comment