Mwanamuziki Nguza Viking (kushoto) na wanawe, kutoka kushoto Papii Nguza, Nguza Mbangu, na Francis Nguza wakiwa katika Mahakama ya Rufani Tanzania, Dar es Salaam kusomewa hukumu ya rufaa yao kupinga adhabu ya kifungo cha maisha jela. Mbangu na Francis wameachiwa huru. MAHAKAMA ya Rufaa Tanzania imeridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa mwanamuziki maarufu, Nguza Viking maarufu kwa jina la Babu Seya na mwanawe, Papii Nguza. Mahakama hiyo imewaachia huru watoto wawili wa Babu Seya, Nguza Mbangu, na Francis Nguza. Naibu Msajili wa mahakama hiyo, Neema Chusi, amesoma hukumu hiyo leo kwa saa mbili jijini Dar es Salaam. Baada ya hukumu hiyo, mahakama ilikuwa kama eneo la msiba kwa kuwa Babu Seya na wanawe walibubujikwa machozi, na ndugu na jamaa zao walilia kwa sauti. Juni 25, 2004 Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kusutu, Dar es Salaam, Addy Lyamuya, aliwatia hatiani Babu Seya na wanawe Papii Nguza ‘Papii Kocha’, Nguza Mbangu na Francis Nguza kwa kupatikana na hatia ya kubaka na kulawiti. Walidaiwa kutenda makosa 10 ya kubaka watoto wenye umri kati ya miaka sita na minane na makosa mengine 11 ya kulawiti watoto wa kike wenye umri huo huo kati ya April na Oktoba 2003 katika maeneo ya Sinza kwa Remmy, Dar es Salaam. |
You Are Here: Home - - Babu Seya kufia jela, wanawe waachiwa
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
0 comments