Kamati ya Mwinyi yawashindwa
Ujasusi watumika kuwinda vigogo wa CCJ
KIWEWE cha kuanzishwa kwa Chama Cha Jamii (CCJ) kinachohusishwa na baadhi ya vigogo maarufu ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinashika kasi huku kamati ya wazee iliyoongozwa na rais mstaafu, Ali Hassan Mwinyi, ikishindwa kumaliza makundi kama ilivyokusudiwa, Raia Mwema limefahamishwa.
Habari za ndani ya CCM na Serikali zinaeleza kwamba kamati ya Mzee Mwinyi imekumbana na vizingiti kadhaa kutokana na baadhi ya vigogo wa juu wa chama hicho kuanza kutegeana katika kufikia makubaliano ya kumaliza tofauti zao.
Tayari CCJ kinaelezwa kuwa chama ambacho kitategemea zaidi matokeo ya kamati ya Mzee Mwinyi na baadhi ya wachambuzi wamekwisha kuonyesha kuwa chama hicho ambacho hata usajili wa muda hakina, kimeitikisa vilivyo CCM ambayo viongozi wake wamekuwa wakitoa kauli za kukiponda.
Pamoja na kuwapo makundi manne ndani ya CCM, makundi mawili ndiyo yanayotajwa kuwa chachu ya misuguano ndani ya chama hicho, yakiongozwa na wanasiasa wawili wazito, Spika wa Bunge, Samuel Sitta na Waziri Mkuu aliyejiuzulu Edward Lowassa kiasi kwamba Kamati ya Mwinyi imekuwa ikiyazingatia zaidi makundi hayo katika kazi yake.
Kundi jingine ndani ya chama hicho ni la viongozi wastaafu ambao ni pamoja na mawaziri wakuu wastaafu; Dk. Salim Ahmed Salim na Jaji Joseph Warioba na Frederick Sumaye ambalo linaelezwa kuwa na nguvu kubwa inayowaumiza vichwa wakubwa ndani ya CCM kiasi cha kuanzisha propaganda ya kuwahusisha wastaafu hao na CCJ.
Frederick Sumaye
Taarifa kutoka kwa watu walio karibu na wastaafu hao zinasema wamekuwa wakishangazwa na kuhusishwa kwao na CCJ katika hatua ambayo wao wanaiona kuwa ya kujaribu kupaka matope historia yao nzuri ya utendaji na uanachama wa CCM.
“ Wanashangaa. Mmoja alitajwa kuwa alikuwa katika mkutano uliounda CCJ siku ambayo yeye alikuwa nje ya nchi. Wamekuwa wakipigiwa simu na waandishi wa habari kutaka maoni yao kuhusu CCJ, na kisha kuandikwa hata kama wanasema hawajui chochote.
“Kati ya wanaotajwa wengine bado ni wajumbe wa Kamati Kuu, sasa katika mazingira ya aina hii unataka hawa wajisikie vipi wanapokwenda kwenye vikao vyao? Hawa ni watu ambao huwezi kuwa na shaka nao juu ya uadilifu wao kama watendaji serikalini na uaminifu wao kama wanachama wa TANU na leo CCM,” alisema mwanasiasa mmoja aliye karibu na wastaafu hao.
Habari pia zinaeleza kwamba Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete, ambaye naye anaelezwa kuwa na kundi lake linalohusisha baadhi ya watu kutoka makundi mengine pia, amependekeza kuwapo maridhiano kati ya kundi la Lowassa na Sitta, pendekezo ambalo limekwama kutokana na kila upande kuhofia ‘kutegwa’.
Habari za karibu na Kamati ya Mwinyi zinasema kwamba baada ya kukutana na wahusika wa pande zote mbili, kundi la Lowassa lilielezwa kukubali maridhiano lakini upande wa kundi la Sitta ulibainisha kwamba hakuna jambo la ugomvi binafsi kati yao bali masuala yanayowagusa Watanzania wote ambao hawajahojiwa na kamati hiyo.
Mhe. Edward Lowassa na Spika Samuel Sitta
“Baada ya kina Lowassa kukubali maridhiano, kina Sitta waliieleza kamati ya Mwinyi kwamba hakuna jambo la kupatanishwa bali kuna masuala ya msingi ambayo yanahusiana na maadili na mustakabali wa nchi ambayo yanapaswa kushughulikiwa kukiokoa chama kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu,” ameeleza mmoja wa watu walio karibu na kamati hiyo.
Habari zinaeleza kwamba Rais Kikwete ameonekana kuwa katikati ya makundi yote mawili huku kila upande ukitaka kiongozi huyo aonyeshe msimamo wake moja kwa moja bila kuhofia upande mmoja wapo.
“Hapo ndipo Kikwete anapoumizwa kichwa maana kila kundi linaamini kwamba Kikwete yuko pamoja nao na wote wanaona kwamba wenzao ndio wakosaji na wanastahili adhabu. Kina Lowassa wanaamini kwamba wenzao wamekisaliti chama na sasa wanawahusisha na kuanzishwa kwa CCJ, huku kina Sitta wakiona kwamba wenzao ni mafisadi waliokichafua chama na hivyo wanastahili kuchukuliwa hatua kuisafisha CCM,” anasema mwanasiasa mwingine.
Misimamo ya makundi hayo mawili ndiyo iliyoisukuma Kamati ya Mwinyi kuwa na mapendekezo yanayobeba maoni ya makundi yote mawili, lakini “ushauri wa Mwenyekiti” ndio ulioisukuma kamati kubadili mapendekezo yake kutoka kwenye kuchukua hatua ama kukemea kuelekea kwenye kupatanisha makundi hayo hasimu.
Habari zinaeleza kwamba CCJ imeitikisa CCM, pamoja na kauli za kujifariji zinazotolewa kupooza makali ya chama hicho ambacho hata usajili hakijapata, kikineemeka kwa gharama za hofu ya ndani ya CCM.
Uchunguzi wa Raia Mwema umethibitisha kwamba vyombo vya dola vimekuwa katika harakati za kuwafuatilia watu wote wanaohusishwa na CCJ hata kwa kutajwa tu, wakiwamo wabunge na hata viongozi wastaafu na wa sasa serikalini.
Kwa mujibu wa habari hizo, nyumba za baadhi ya watu wanaohofiwa kuwa nyuma ya CCJ zimewekewa ukachero wa hali ya juu ikiwa ni pamoja na kuwekwa vifaa ama watu maalumu ndani na nje ya maeneo wanayoishi na kufanyia kazi na baadhi ya maeneo hata watu kuzunguka ufukweni mwa bahari karibu na makazi hayo.
“Tanzania sasa imekuwa kama nchi nyingine za Afrika zinazoendesha siasa za kibabe na huko tunakoelekea hali itakuwa mbaya zaidi. Hebu fikiria sasa CCJ imesababisha watu waanze kuogopa hata kutembeleana. Inatisha sana, wageni wakija unawaambia wasizidi wawili maana mtaambiwa mnafanya kikao,” anasema Mbunge mmoja wa CCM anayetajwa kuhusishwa na CCJ.
Imeelezwa kwamba kwa sasa watu ambao vigogo ndani ya CCM wanawahofia wanaotajwa kuwa ndani ya kundi la Sitta na lile la mawaziri wastaafu, kutokana na nguvu zao kisiasa na wanasiasa hao wameelezwa kufuatiliwa kwa karibu huku baadhi ya wafuatiliaji wakidhihirisha waziwazi na wengine wakifanya hivyo kijasusi.
Mbali ya wanasiasa, Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa na watendaji wake nao wamejikuta wakitakiwa na vyombo hivyo kutoa maelezo ya kina kuhusiana na wahusika wakuu wa chama hicho na historia zao hali ambayo inatishia uhai wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa nchini leo zaidi ya miaka 18 tokea kuhalalishwa.
Wakati vyombo vya usalama vikiwa katika harakati hizo, baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM, akiwamo Katibu Mkuu wake, Yussuf Makamba, wameendelea kutoa kauli za kupuuza kuanzishwa kwa chama hicho na kuhusishwa kwake na vigogo mashuhuri wa CCM.
Katibu Mkuu CCM, Yussuf Makamba
Makamba amenukuliwa na baadhi ya vyombo vya habari nchini akisema chama chake hakitishiki na kuanzishwa kwa CCJ lakini pia kwamba kama kuna vigogo wanaokusudia kuhama CCM wakifanya hivyo watakuwa wamejimaliza kisiasa.
Mbali na Makamba kiongozi mwingine wa CCM aliyetoa kauli ya namna hiyo ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Kapteni (mstaafu) John Chiligati, huku baadhi ya vyombo vya habari vikiwamo vinavyotajwa kuegemea kundi mojawapo kati ya mawili makubwa yanayokinzana ndani ya CCM, vikitumika kuwahusisha wenzao wa kundi jingine.
Makamba na wenzake wamekuwa wakikwepa hali ya mambo kwamba makundi mawili makubwa ndani ya CCM yamekuwa yakijitofautisha katika kile kinachotajwa kuwa ni vita dhidi ya ufisadi, kundi moja likipinga ufisadi na kutaka chama hicho kisimamie misingi ya kuanzishwa kwake na misimamo ya waasisi wa chama hicho, Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume.

0 comments