Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - MATUKIO MAKUBWA YALIYOTOKEA TAREHE 31/12/209 KABLA YA MWAKA MPYA 2010

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Kawawa ametuacha
Thursday, 31 December 2009
Image Huu ni msiba mkubwa kwa taifa tunapofunga mwaka kwa kumpoteza mmoja wa mashujaa waliotuletea uhuru. Rashid Mfaume Kawawa amefariki leo asubuhi kwenye hospitali ya Muhimbili alipolazwa tangu jana kwa matatizo ya kiafya akiwa na umri wa miaka 83. Rais Jakaya Kikwete ametangaza siku saba za maomboleza ambapo bendera itapepea nusu mlingoti. Kalale kwa amani Baba
Waliotengeneza habari 2009
Thursday, 31 December 2009

Image RAIS JAKAYA MRISHO KIKWETE Utawala wake mwaka huu umekuwa kwenye macho ya wengi hasa kwenye vita dhidi ya ufisadi na umaskini. Amekuwa akipingwa na badhi ya wazee wa CCM. Ujihusishaji wake kwenye jamii umedhihirika kwa hali ya juu

Image RAIS BARACK OBAMA Tuzo yake ya Nobel imeibua mjadala mkubwa duniani. Alianza kutengeneza habari baada ya kujitosa kugombea urais wa Marekani na kuchukua mwanzoni mwaka huu.Harakati zake za kuleta udiplomasia wa kimataifa zimeboresha mahusiano kati ya Marekani na nchi nyingine

HASHIM THABEET Mtanzania wa kwanza kucheza kwenye ligi ya mpira wa kikapu Marekani. Hashim (futi 7'3) alichaguliwa kucheza ligi hiyo kubwa zaidi ulimwenguni katikati ya mwaka na kuiweka Tanzania katika ramani ya kimataifa. Mapumziko yake mafupi nchini yalivuta ya vyombo vya habari

STEVEN KANUMBA Stori za jamaa huyu kuchemka kimombo wakati akiwa kwenye jumba la Big Brother zilisikika na kuonekana sana kwenye vyombo vya habari ingawa mwenyewe alijitokeza na kupinga madai hayo.Filamu zake bado zimeendelea kutamba na kumfanya awe juu maradufu

Umodo si rahisi
Thursday, 31 December 2009

Image Lisa Jensen, ambaye kwa sasa anafanya uanamitindo chini ya Elite Model Agency, ameongea na Bongo5 na kusema fani ya mitindo nchini India si rahisi kama inavyochukuliwa Bongo

Tamasha la msamaha
Thursday, 31 December 2009

Image Kwa mara ya kwanza nchini na pengine duniani kote lilifanyika Tamasha la kusameheana kwenye ukumbi wa Mlimani city jana usiku. Kwa mujibu wa muaandaaji ambaye alijitambulisha kama Mr Forgiveness, tamasha hilo lenye lengo la kuwapatanisha waliogombana, ni moja ya hatua za kufanya siku ya msamaha itambulike duniani kama zinavyotambulika siku za wajinga na wapendanao

Image Bendi ya Mrisho Mpoto ilikuwepo kutumbuiza na ingawa Wahu naalikuwa kwenye listi ya waburudishaji, hakuweza kutokea

Image Shoti and Hasara.......jamaa wanachekesha sana hawa

Tags:

0 comments

Post a Comment