IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
Sakata la mgombea binafsi wa nafasi ya Urais na Ubunge limechukua sura mpya baada ya Jaji Mkuu wa Tanzania, Augustino Ramadhani kupanga majaji saba kusikiliza rufaa iliyokatwa na Serikali kupinga kuwepo kwa mgombea huyo.
Kesi hiyo ni ya aina yake kwani rufaa nyingi husikilizwa na jopo la majaji watatu si saba kama ilivyo kwa rufaa hiyo namba 45 iliyokatwa na Mwanasheria Mkuu wa Serikali dhidi ya Mchungaji Christopher Mtikila.
Rufaa imepangwa kusikiliza Februari 8, mwaka huu mbele ya majaji hao saba wa Mahakama ya Rufaa.
Mchungaji Christopher Mtikila alifungua kesi ya kikatiba namba 10 ya mwaka 2005 katika Mahakama Kuu ya Tanzania akiomba baadhi ya vifungu vya katiba vifanyiwe marekebisho kwa sababu havitendi haki.
Vifungu hivyo ni namba 21(i) kinachosema kwamba bila kuathiri masharti ya Ibara ya 5, 39 na 67 ya katiba na sheria za nchi kuhusina na masharti hya kuchagua na kuchaguliwa au kuteua na kuteuliwa kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi, kila raia wa Jamhuri ya Muungano wa Tanznaia anayo haki ya kushiriki katika shughuli za utawala wa nchi.
Mtu huyo anaweza kushiriki moja kwa moja au kwa kupitia wawakilishi waliochaguliwa na wananchi kwa hiari yao au kwa kuzingatia utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa sheria.
Pia kifungu namba 39 (1) kinachosema kwamba mtu hastahili kuchaguliwa kushika kiti cha rais wa Jamhuri ua Muungano isipokuwa ni mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa.
Kifungu namba 39 (2) bila kuingilia uhuru wa mtu kuwa na maoni yake, kuamini dini atakayo, kushirikiana na wengine pia kushiriki shughuli za umma kwa mujibu wa sheria za nchi, mtu yoyote hatakuwa na sifa za kuchaguliwa kushika kiti cha Rais kama si mwanachama na mgombea aliyependekezwa na chama cha siasa.
Aliomba kifungu namba 67 pia kifanyiwe marekebisho ambacho kinasema kwamba kwa mujibu wa sheria za nchi ikiwa mtu si mwanachama wa chama chochote cha siasa hatakuwa na sifa za kuchaguliwa na kuteuliwa kuwa mbunge.
Mchungaji Mtikila aliomba vifungu hivyo vifanyiwe marekebisho na Mahakama iruhusu kuwepo kwa mgombea binafsi wa nafasi ya urais na ubunge.
Baada ya kusikiliza maombi hayo Jopo la Majaji watatu akiwemo Jaji Amir Manento Salum Massati na Jaji Mihayo lilitoa hukumu Mei 5, mwaka 2006 na kukubaliana na hoja za Mchungaji Mtikila kwamba vifungu hivyo havitendi haki hivyo vinastahili kufanyiwa marekebisho na kuruhusu mgombea binafsi.
Uamuzi huo ndio uliofanya Serikali kukata rufaa hiyo ambayo inatarajiwa kusikiliza Februari.
You Are Here: Home - - Majaji 7 kutegua ishu la mgombe binafsi!
0 comments