Obama akiri dosari za usalama
Rais Obama amekiri kwamba maafisa wa idara ya ujasusi wa Marekani walikusanya taarifa za kutosha kumzuia raia wa Nigeria kusafiri na ndege aliyojaribu kulipua siku ya krisimasi.
Hata hivyo maafisa hao walipuuza taarifa hizo.
Akiongea baada ya kukutana na washauri wake wa usalama Rais Obama amesema taarifa za kijasusi sharti zitiliwe maanani.
Rais huyo ameongeza kulikuwa na taarifa za kutosha kuhakikisha kuwa Umar Farouk Abdul Mutallab, hakubaliwi kusafiri na ndege hiyo.
Obama hata hivyo ameihakikishia dunia kwamba jaribio hilo halitabadilisha mpango wa utawala wake wa kufunga kizuizi cha Guantanamo Bay.
0 comments