Picha zifuatazo zinaonyesha jinsi tukio zima la mazishi ya hayati Rashid Mfaume Kawawa ‘Simba wa Vita’ yalivyokuwa jioni hii nyumbani kwake Madale nje kidogo ya jiji la Dar es salaam.
..Rais Amani Karume akitia saini kitabu cha maombolezo
...Waziri Mkuu Mh. Pinda akitoa hotuba fupi
... ni wakati wa kumsomea dua marehemu
...kila mtu alihudhuria
...Mh. Ben Mkapa na Pius Msekwa
..Wakati wa swala ya marehem
...picha za kumbukumbu
...kwa heshima zote amezikwa
...Ulale mahala pema peponi
..haya ndiyo makazi ya milele ya Mzee wetu Rashid Kawawa.
Umati wa wananchi, viongozi wa serikali na vyama mbalimbali, jana Ijumaa, walikusanyika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaam kumuaga muasisi wa taifa hili la Tanzania, Rashid Mfaume Kawawa maarufu ‘Simba wa vita.’ Tukio hilo liliongozwa na Rais Jakaya Kikwete na kufuatiwa na viongozi wengine wa serikali.
Mjane wa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mama Maria, akiingia viwanja vya Karimjee kwaajili ya shughuli za kuaga mwili.
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akitia saini kwenye daftari la wageni lililokuwa mahali hapo.
Mwenyekiti wa Tanzania Labor Party, Augustino Mrema alivyowasili.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kushoto) akiwasikiliza mabosi wake: Kamishna Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Said Mwema (Kulia) na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Davis Mwamunyange (mwenye gwanda la kijani katikati).
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, William Lukuvi (katikati) akimuongoza Rais mstaafu wa awamu ya pili, Ally Hassan Mwinyi.
Aliyekuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Omary Mahita akiwa msibani hapo.
Hivi ndivyo Rais Jakaya alivyowasili viwanja vya Karimjee kwaajili ya kuaga mwili.
Mwili wa Simba wa vita ukiingizwa kwa heshima viwanja vya Karimjee kwaajili ya kuagwa.
Maaskari wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) wakiingiza mwili Simba wa vita viwanjani hapo.
Viongozi mbali mbali nchini akiwemo Pius Msekwa (wa mbele) na Makamba (katikati) wakiaga mwili wa marehemu Kawawa.
0 comments