Mchezaji wa Togo Emmanuel Adebayor |
Vyombo vya habari vinasema wanachama 2 wa timu ya Togo na dreva wa basi wameuawa katika shambulio hilo. Watu wengine 9 wamejeruhiwa. Golikipa Obilale Kossi na beki Sege Akakpo wa timu hiyo ni miongoni mwa majeruhi.
Nalo Shirikisho la Soka barani Afrika limesema mashindano ya Kombe la Mataifa ya Afrika yataendelea kama ilivyopangwa.
Serikali ya Angola imelaani shambulio hilo na imeahidi kuimarisha ulinzi wa usalama wakati wa michezo hiyo. Kundi la FLEC linalogombea uhuru wa eneo la Cabinda limedai kuwa ndio lililohusika na shambulio hilo na limetishia kufanya mashambulio mengine wakati wa michezo hiyo.
Wachezaji wawili wa Togo walifyatuliwa risasi na kujeruhiwa katika mkoa wa kaskazini wa Cabinda siku ya ijumaa.
Waandaaji wanasisitiza kuwa michuano itaendelea na kwamba wataimarisha usalama.
Lakini mchezaji wa Togo Alaixys Romao ameliambia gazeti moja la lugha ya kifaransa L'Equipe: "Tunazungumza na timu zengine katika kundi letu kuzishawishi zisusie."
Katika mechi yao ya kwanza siku ya Jumatatu Togo ilipangiwa kucheza na Ghana huko Cabinda na wachezaji wa timu hiyo inayojulikana kama Black Stars wamesema kuwa wako tayari kuendelea kucheza.
Ivory Coast na Burkina Faso ni timu zengine zilizopangwa katika kundi B.
0 comments