Subscribe to receive latest Updates

Online :

You Are Here: Home - - Marekani yahaha usafiri wa ndege

IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII: counter
Ramani ya Marekani
FBI yasema halikuwa tukio la kutisha
Wasiwasi tena kwenye ndege Marekani
Ndege hiyo ilikuwa pia inasafiri kutoka Amsterdam, Uholanzi hadi Detroit, Marekani.Siku moja tu baada ya jaribio la kulipua ndege huko Marekani kutibuliwa kulikuwa na wasiwasi wakati abiria kwenye ndege nyingine alipokawia msalani.

Rubani wa ndege ya kampuni ya Northwest Airlines alituma ombi la dharura kutokana na kile kilichoelezwa kuwa abiria msumbufu.

Taarifa zasema abiria mhusika, ambaye pia ni raia wa Nigeria, alikumbwa na kichefuchefu na ikambidi kwenda msalani.

Lakini kukawia kwake kwenye choo kwa zaidi ya saa nzima kulizusha wasiwasi mkubwa kwenye ndege hiyo kiasi cha kumfanya rubani kutuma ombi la dharura.

Abiria huyo alikamatwa na baada ya kupekuliwa hakupatikana na kifaa chochote hatari.

Hata hivyo maafisa wa shirika la uchunguzi la Marekani, FBI, walisema kwamba tukio hilo halikuwa la kutisha.

Mnamo siku kuu ya Krismasi, abiria karibu 300 waliponea chupuchupu wakati kijana wa miaka 23, Farouk Umaru Abdulmutallab, akiwa amejifunga mabomu alijaribu kujilipua.

Rais Barack Obama aliarifiwa kuhusu tukio hilo akiwa likizoni huko Hawaii.

Tags:

0 comments

Post a Comment