You Are Here: Home - - EU kuipatia Tanzania bilioni 749/=
IDADI YA WATU WALIOSOMA HABARI HII:
UMOJA wa Ulaya (EU), umesaini makubaliano ya kuisadia Tanzania Sh bilioni 749.5 (Euro milioni 379.5) kuiwezesha kutekeleza shughuli za maendeleo ili kupunguza umasikini na kuharakisha kasi ya ukuaji wa uchumi.
Fedha hizo pia zitaiwezesha Tanzania kutekeleza Malengo ya Maendeleo ya Milenia (MDG) na kuimarisha sekta ya usafiri nchini.
Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhan Khijjah, na Mkuu wa Tume ya Ulaya, Balozi Tim Clarke wamesaini mkataba huo Dar es Salaam.
Waziri wa Fedha na Uchumi, Mustafa Mkulo, ameshuhudia kusainiwa kwa makubaliano hayo.
Khijjah amesema katika hafla hiyo kwamba, kiasi hicho cha fedha kitasaidia kutekeleza malengo yaliyokusudiwa ya kukuza uchumi.
Balozi Clarke, amesema,Tanzania ni miongoni mwa nchi saba duniani zilizonufaishwa na msaada huo ulitolewa na Umoja wa Ulaya utakaosaidia kuleta mafanikio katika kipindi cha miaka sita ijayo.
Amesema, ni vema kwa Serikali ihakikishe inaondoa vikwazo vinavyokwamisha maendeleo ikiwa ni pamoja na matumizi mabaya ya rasilimali,rushwa, matumizi mabaya ya madaraka kwa baadhi ya watendaji, ucheleweshaji wa kesi za rushwa na ucheleweshaji wa kesi za ukiukwaji wa haki za binadamu.
Waziri Mkulo amesema, Serikali ipo makini kuhakikisha inashughulikia vikwazo vinavyokwamisha maendeleo iki ni pamoja na kupambana na rushwa.
0 comments